Kiongozi wa Boko Haram, SHEKAU bado yu Hai
Kiongozi wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Nigeria, Boko Haram, amekanusha ripoti kwamba ameuwawa au kutolewa katika uongozi.
Katika
rikodi ya sauti inayoaminiwa ni ya Abubakar Shekau, anaeleza kuwa ni
uongo ripoti kwamba amefariki, amelemaa au ni mgonjwa.
Juma
lilopita rais wa Chad, Idriss Deby, alisema kuwa Boko Haram imemteua
kiongozi mpya na kuzusha tetesi kwamba Bwana Shekau ameuawa.
Ujumbe wake huo umewekwa katika mitandao ya kijamii na ulilengwa kwa kiongozi wa Islamic State, Abu Bakr al-Baghdadi.
Awali mwaka huu, Boko Haram ilitangaza kuwa ni tiifu kwa IS.
Post a Comment