Mkutano wa Baraza la Mawaziri, wa Nchi za Maziwa Makuu Wafanyika ZANZIBAR
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuwakaribisha nchini
wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika
katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu
(RECSA) kabla ya kufungua kikao cha wajumbe hao kinachofanyika katika
Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar. Lengo la kikao hicho ni kujadili masuala
mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa
Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout,
Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini,
Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa
Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na
Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika chumba cha
mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na
Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni
Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan,
Uganda, Sudan, Sudan ya Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na
Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya
Sea Cliff, Zanzibar ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe (hayupo pichani) ndio Mwenyekiti wa Baraza hilo, hata hivyo
katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima (kulia meza kuu) anamuwakilisha katika kikao hicho. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini, Pereira Ame Silima (kulia)
akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Uganda ambaye pia ni Makamu
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi James Baba (katikati) na Mjumbe wa
Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani
nchini Rwanda, Balozi Munyabagisha Valeus, wakisoma taarifa za masuala
mbalimbali ya jinsi ya Kupambana ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa
Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout,
Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini,
Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Baraza hilolimekutana
katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi nchini, Pereira Ame Silima
(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza
hilo ambalo nchi zake wanachama ni Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea,
Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya
Kati, Somalia na Tanzania. Wajumbe hao wamekutana katika Hoteli ya Sea
Cliff, Zanzibar leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Post a Comment