Bi CAROLINA CHILELEL, aibuka na Milioni 20, Shindano la Mama SHUJAA wa Chakula
Mshindi wa Shindano lala Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa Nne mwaka 2015 Calorina Chilele Muda mchache Baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Afisa
Kilimo Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dkt. Kissa Kajigili ,
akiwapongeza Oxfam kwa kuandaa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na
washiriki wote kwa ujumla walioshiriki katika Shindano hilo, Pia
alimpongeza Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2015 Carolina Chilele na
kumtaka awe mfano bora pia akawe chachu ya kuinua kilimo na kuwasaidia
wenye uhitaji yaani wakulima wanawake wadogo wadogo, Mwisho aliwaomba
Oxfam waendelee na Shindano hili muhimu.
Jackson Yusuph Mzumba Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibweni akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Serikali ya Kijiji cha Kisanga.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisarawe Bw. Ellioth Phillemon
Mwasambwite akiwashukuru Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
2015 , na kuwaaaga rasmi, pia kumpongeza Mshindi wa Shindano hilo msimu
wa Nne Bi. Carolina Chilele , Mwisho aliwapongeza Oxfam kwa kuanzisha
shindano endelevu kwa Maendeleo ya wakulima hasa wanawake.
Mmoja
wa akina mama ambao walikuwa wanakaa na Washiriki wa Shindano la Mama
Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Kisanga Bi. Sophia Shomvi akitoa
neno la Shukurani kwa washiriki hao kwa jinsi walivyo kaa vizuri pamoja
na pia kuwaachia elimu kubwa wanakijiji hao. Mwisho alitoa neno la
Kuwaaga Rasmi.
Kiongozi
wa Timu ya Urasimishaji ardhi vijijini kutoka Wizara ya Ardhi nyuma na
Maendeleo ya Makazi Bw. Swagile Msananga akiwapongeza washiriki wa
Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, pia kwa mshindi wa Shindano
hilo kwa msimu wa Nne 2015 Bi. Carolina Chilele kwa ushindi wake na
kumtaka kuwa mfano Bora kwa jamii kwa ujumla, Pia alisisitiza watu sio
kuwa tu na ardhi lakini pia kupata umiliki wa ardhi walizonazo.
Baadhi
ya Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakipewa tuzo
za ushiriki wao na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster.
Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2015 msimu wa Nne Carolina Chilele akipongezwa na washiriki mwenzake.
Picha ya pamoja.
Baadhi
ya Wageni waalikwa , Wafanyakazi wa Oxfam, Ndugu jamaa na Marafiki
wakiwa katika Sherehe za Fainali za Shindano la Mama shujaa wa Chakula.
Bi.
Hawa Mkata aliyekuwa Mshiriki kutoka Mtwara akitoa neno la Shukurani
kwa wanakijiji wote ambao waliishi nao Kijijini kwa Muda wa Siku zote
21, na zaidi zile Familia ambazo wao wamekuwa nao kwa kipindi chote cha
Shindano hilo, Mwisho aliwaomba washiriki wenzake kujua kuwa wote ni
washindi lakini mmoja ndio kawawakilisha kwa kuchukua zawadi ile ya
Milioni Ishirini.
Eva
Mgeni, Mshiriki kutoka Bagamoyo Kutoka Mkoa wa Pwani, Akitoa Shukurani
zake kwanza kwa Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow ambayo kauli mbiu
yake ni kuwekeza kwa wakulima wadogo wadogo wanawake inalipa kwa
kuendesha shindano hili na kuwa kupitia washiriki wa shindano hilo
wamejifunza mambo mengi na ya kimaendeleo, Mwisho aliwashukuru
wanakijiji wote kwa ushirikiano wao na Moyo wa Ukarimu katika kipindi
chote wakiwa Kijijini.
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa salam zake za Shukurani kwa
wote waliofanikisha shindano la Mama shujaa wa Chakula kwenda vizuri
tangu mwanzo mpaka mwisho, aliwashukuru wanakijiji cha Kisanga kwa
kukubali kwao shindano lifanyike katika kijiji hicho pia aliwapongeza
washiriki wote wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula na kuwasihi kuwa
wote walikuwa ni washindi, Mwisho alichukua nafasi hiyo kumpongeza
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 na kumsihi aende kuwa
mfano wa kuigwa kwa wakulima wenzake pia akawe Balozi mzuri na
kuiwakilisha vema Oxfam.
Mshindi
wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne akitoa neno la
Shukurani kwa ushindi alioupata , Ameshukuru shirika la Oxfam kwa
kuendesha shindano hilo na kuahidi kuwa atakwenda kuwa Balozi mzuri na
kusema kuwa washiriki wote ni washindi na yeye amepata zawadi hiyo
kuwawakilisha wote.
Burudani ikiendelea.
.....................................
Na Mwandishi wetu
.....................................
Na Mwandishi wetu
Hatimaye Shindano la Mama Shujaa wa Chakula shindano linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia Programu yake ya Grow ambapo kauli mbiu ni Wekeza kwa wakulima wanawake wadogo wadogo inalipa lafika tamati.
Ambapo kulikuwa na mchuano mkali kati ya washiriki 15 ambao walikuwa katika Kijiji cha Kisanga Wilayani Kisalawe Mkoani Pwani wakiwa na shughuli mbalimbali za Kilimo ambazo zililenga hasa katika kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wanawake wadogo wadogo.
Washiriki hao walikaa kijijini kwa muda wa siku 21 hatimaye kufikia kumpata mshiriki mmoja ambaye amejishindia kiasi cha Tsh 20,000,000 fedha ambazo zitanunua pembejeo za Kilimo.
Fainali hizo zilifanyika katika Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam
Post a Comment