Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto Kuhusu Malaria Kuanza Rasmi AGOSTI 21
Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu
Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii
akiwahutubia Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya
kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea umuhimu waUtafiti wa Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya
kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za
Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo
ya awali wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo
iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Wasimamizi, Wahariri na
Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa
mwaka 2015 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa hafla
fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu
Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasimamizi,
Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria
Tanzania wa mwaka 2015 mara baada ya kufunga mafunzo ya utafiti huo
wilayani Moshi, Kilimanjaro.
…………………………………………………………………………………….
Na Veronica Kazimoto, Moshi
Wito umetolewa kwa viongozi
wote wa Serikali katika Ngazi zote na wananchi kwa ujumla kutoa
ushirikiano kwa Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria utakaoanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015.
Wito huo uletolewa leo na
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.
Ahmed Makuwani wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo
iliyofanyika wilayani Moshi, Kilimanjaro.
“Ninawaomba Wananchi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi, Wasimamizi na
Wahaririwatakaoshiriki zoezi la kukusanya Takwimu za Utafiti wa Afya ya
Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ili kupata taarifa muhimu na
sahihi kwa ajili ya kupanga Mipango na Sera endelevu za Sekta ya Afya
katika nchi yetu, amesema Makuwani”.
Dkt. Makuwani amesema kuwa
taarifa zitakazokusanywa kwa wananchi kwa ajili ya utafiti huo zitakuwa
ni siri na zitatumika kwa shughuli za Kitakwimu tu na wala hazina
uhusiano wowote na Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
kwa upande
wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
amesema utafiti huu wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015
unalenga kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika katika
kutathmini malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga mikakati
mipya.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa
mara nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria
wa mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2010. Utafiti
huu utaanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015 kwa nchi nzima na utamalizika
mwishoni mwa Mwezi Februari 2016.
Post a Comment