Mafunzo kwa Madereva wa Mabasi ya Mwendo kasi Yazinduliwa Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, akijaribu kuendesha moja ya basi la mwendo wa haraka wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam.
Babasi ya wendo wa haraka yaliyoingia nchini kutoka nchini china.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akizungumza katika uzinduzi huo.
Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Askari wa usalama barabarani wakichukua taswira za mabasi hayo.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Nchini, Mohamed Mpinga (kushoto), akibadilishana mawazo na wadau wa usafirishaji kabla ya uzinduzi huo.
Meza kuu hiyo ikiwa na viongozi mbalimbali.
Msemaji wa Mradi wa DART, Sabri Mfuruki, akizungumza (katikati) akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji, William Masanja.
Wanahabari wakichukua taarifa katika uzinduzi huo.
Wakufunzi wa kutoa mafunzo kwa madereva hao kutoka China wakitambulishwa.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Massaburi ndani ya mchuma wakati wa uzinduzi huo. Hapo wanakwenda Kimara kutoka Ubungo na kisha kurudi Ubungo 'Hakika ni Raha tupu'
Wanachi na wadau wengine wakiangalia mabasi hayo.
Dotto Mwaibale
MADREVA waliobahatika kuanza kupata mafunzo ya kimataifa ya kuendesha mabasi ya mwendo wa haraka chini ya mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka (DART), wametakiwa kuzingatia mafunzo hayo kwa makini.
Mwito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, wakati akizinduzi mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka uliofanyika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo Dar es Salaam leo.
"Mafunzo mtakayopata nawaombeni muyapokee kwa bidii na umakini mkubwa kwani yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa" alisema Ghasia.
Ghasia alisema mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani kwa mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na kuwa mafunzo hayo hayatalenga tu kuendesha magari bali pia namna ya kuwahudumia wateja.
Alisema anaamini mafunzo hayo yatawejengea madereva hao weredi na dinadhamu katika kazi yao ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kuandamwa na utovu wa nidhamu na kutotii sheria za barabarani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alisema mradi huu wa mabasi yaendayo kasi ni mradi wa aina yake hapa nchini na barani Afrika kwa ujuma na utatoa fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi na ni msingi wa maendeleo ya nchi.
Mahitaji ya madereva wanao hitajika katika mradi huo ni 330 na kuwa mradi huu ulioanza ni wa awamu ya kwanza na utakuwa wa awmu tano.
Post a Comment