Timu ya Taifa ya BASEBALL yakabidhiwa Vifaa vya Mchezo huo
Bw. Alferio Nchimbi Katibu wa
Chama cha Mchezo wa Baseball na Softball Tanzania akikabidhi vifaa vya
michezo kwa wachezaji wa timu ya mchezo huo ya Tanzania inayotarajia
kuondoka kesho kuelekea nchini Uganda kwa ajili kambi ya mafunzo ya Meja
League Base Ball Training Camp For Tryout (MLB) yatakayofanyika kuanzia
tarehe 23-25 Agosti 2015.
........................................................
Wachezaji watakaochaguliwa kutoka
katika kambi hiyo watakwenda nchini Afrika Kusini kwa kwa mafunzo ya
wiki mbili na baadaye wachezaji watakaochaguliwa kutoka kambi ya mafunzo
ya Afrika Kusini watakwenda katika mafunzo kama hayo nchini Marekani
kwa ajili ya kupata mafunzo zaidi ya mchezo huo na Scholarship ya kusoma
nchini humo.
Wachezaji waliochaguliwa katika
timu hiyo ya taifa kwenda nchini Uganda ni Abdallah Abdallah kutoka
Shule ya Sekondari ya Al Muntazir, Pius Cheka kutoka Sekondari ya
Kibasila, Martin Cosmas kutoka Sekondari ya Azania, Juma Fikiri na
Leodgar Leonidas kutoka sekondari ya Azania. Timu zitakazoshiriki
katika mafunzo hayo ni Tanzania, Kenya na Uganda.
Katika Picha kutoka kushoto ni
Mwalimu Marck Hatia , Juma Fikiri, Martin Cosmas na Leodgar Leonidas
wachezaji wa timu hiyo waliopokrea vifaa hivyo kwa niaba ya wenzao.
Post a Comment