Serikali Imekanusha Madai ya Chadema Kutumia Uwanja wa Taifa Kuzindulia Kampeni !
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
akikanusha kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua kampeni zake
siku ya tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam. Kanusho hilo
lilitolewa katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia
taarifa kutoka Serikalini kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa
kuzindua kampeni zake siku ya tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es
Salaam. Kanusho hilo lilitolewa katika Ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) uliopo jijini Dar es Salaam.
.....................................................................
Na Benedict Liwenga,Maelezo
SERIKALI imekanusha taarifa
zilizojitokeza kwenye Vyombo vya habari yakiwemo magazeti na mitandao ya
kijamii kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitafanya
mkutano hadhara Uwanja wa Taifa Dar es Salaam tarehe 22 Agosti, 2015.
Akizungumza na vyombo vya
habari jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene
alisema serikali haijatoa ruhusa kwa chama chochote cha siasa kutumia
uwanja wa taifa kwa ajili ya shughuli za kisiasa.
Alikiri kwamba ni kweli kwamba
CHADEMA waliiandikia Wizara tarehe 12 Agosti, 2015 kutaka kutumia uwanja
wa taifa katika uzinduzi wa kampeni lakini ombi lao lilikataliwa kwa
maelezo kwamba uwanja ule kwa mazingira ya sasa hauruhusiwi kutumika kwa
ajili ya mihadhara ya vyama vya siasa.
“kwa kipindi haturuhusu uwanja
wa taifa kutumika kwa mihadhara ya kampeni za vyama vya siasa. Uamuzi
huu unalenga kuweka uwanja katika mazingira rafiki ya michezo na kuepuka
athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na mihemuko ya kisiasa”
alisema Bwana Mwambene.
Mwambene ameeleza kuwa,
Serikali imeamua uwanja huo ubaki kwa ajili ya kufanyia shughuli zake za
msingi za kimichezo ili kuepuka mihemuko na athari yoyote inayoweza
kujitokeza kutokana na hamasa za kisiasa.
“Ni kweli kwamba tulipata barua
ya Chadema kuomba Uwanja kutumika kwa ajili ya mhadhara ya kisiasa wa
CHADEMA hasa kuzindua Kampeni zao kwenye Uwanja tayari tumeshawaandikia
kuwaarifu kuwa Uwanja ule hauwezi kutumika kwa ajili ya shughuli zozote
za kisiasa” alisema Bwana Mwambene.
Alisema vyama vyovyote vitakavyoomba kutumia Uwanja ule kwa shughuli za kisiasa havitaruhusiwa.
Post a Comment