Peremende Zenye Bangi !!!... Zinauzwa nchini KENYA ?
Wizara ya afya nchini kenya imetoa orodha ya peremende, keki na biskuti bidhaa ambazo inadai zimewekwa bangi.
Katika kile ambacho kinatarajiwa kuwashanga wazazi, barui ambayo 
ilitiwa sahihi kwa niaba mahabara ya serikali, ilisema kuwa baadhi ya 
sampuli 176 zilizochukuliwa kwa peremende maarufu , keki na mandazi 
zilipatikana zikiwa na bangi baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Licha ya watoto kuvipenda 
bidhaa hizo serikali inataka vipiwe marufuku na kuondolewa kabisa 
madukani na pia wachuuzi kuzuiwa kiziuza.
Kupitia kwa barua kwenda
 kwa wakuu wa afyua wa kaunti zote 47 nchini Kenya, wizara ya afya 
imewaamrisha maafisa kukagua maduka yote, maduka ya jumla na sehemu 
zingine bidha hizo zinaweza kupatikana.


Post a Comment