Header Ads

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani akagua Ujenzi Nyumba za Askari Magereza

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na Mshauri wa Kitengo cha Utafiti wa Udongo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (BICO,UDSM), Dk. Dalmas Nyaoro, baada ya kuwasili eneo la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Magereza ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika  katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akisaini dafrari la wageni baada ya kuwasili kwenye Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari  Magereza unaoendelea katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Mradi huo unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika. 

Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), wakati Katibu Mkuu alipotembelea kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la  Magereza, ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la  Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu Mkuu wa mradi huo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Julius Chego.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa Kaunda suti), akiteta jambo na Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa wakati  alipotembelea kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la  Magereza, ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. 

No comments

Powered by Blogger.