Wachimbaji wa Madini Watakiwa Kujipatia Elimu na Teknolojia Sahihi
........................
Na Daudi
Manongi, MAELEZO
Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa ametoa wito kwa wachimba wadogo wadogo wa madini kuongezea
juhudi katika uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na kujipatia elimu ya
uchimbaji sahihi wa madini na kutumia
teknolojia nzuri ambayo itawasaidia kuongeza tija katika shughuli zao.
Profesa Ntalikwa
ameyasema hayo wakati akifungua mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini wanaojihusisha na
uchimbaji ambao sio rasmi na mdogo uliofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam.
“Mimi wito wangu kwa
wachimbaji hawa ni kwamba nawaomba wajipatie elimu na teknolojia sahihi ili
waweze kujiongezea kipato katika uchimbaji huu”,Alisema Prof Ntalikwa.
Aidha Katibu Mkuu uyo
aliwataka wachimbaji wadogo wadogo hao kuwasiliana na Baraza la Taifa la
uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) kwa ajili ya kuwasaidia sehemu ambazo ambazo
wanaweza kupata mitaji maana suala la mtaji ni muhimu sana ili waweze kuboresha
shughuli za uchimbaji.
Pia amesema kuwa serikali imeanza kutoa ruzuku kwa awamu kwa
wachimbaji hawa wadogo wa madini na hivi sasa wanajipanga kutoa awamu ya tatu
ya ruzuku ikiwa na lengo ya kuwasaidia
kununua vifaa vya uchimbaji na teknolojia sahihi itakayorahisisha uchimbaji wa
madini na kuongeza kuwa kwa sasa wameshapokea maombi kutoka kwa wachimbaji
mbalimbali na wanayafanyia kazi ili wapate washindi watakaojipatia ruzuku.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa amesema kuwa wao kama baraza
watatengeneza programu ya jinsi ya kupata uongozi kwa wachimbaji hao ambao
utasaidia kuwakilisha mawazo yao serikali na pia program ya kuwajengea uwezo
pale ambapo wachimbaji hawa wana mapungufu na pia kuwaunganisha na masoko kama
vile viwanda vya ndani ili visinunue malighafi kutoka nje na badala yake
wanunue hapa nchini malighafi yanatotokana na uchimbaji wa madini.
Post a Comment