Header Ads

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA BARAZA LA WAUGUZI NA WAKUNGA


Picha ya pamoja ya mgeni rasmi Waziri wa Afya
Rashid Seif na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga mara baada ya uzinduzi
rasmi.
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar       

Waziri wa Afya  wa Zanzibar Rashid Seif ameliagiza Baraza la Wauguzi na 
Wakunga Zanzibar kusimamia kwa karibu watendaji wa kada hiyo ili  wawezekuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa Baraza Wauguzi na Wakunga katika Chuo cha  Sayanzi ya Afya Mbweni, Waziri Rashid Seif amesema wauguzi na wakunga ni walezo wanaoshughulikia matatizo ya watu hivyo wanatakiwa kutekeleza wajibu wao.
 
Amesema wananchi wanapofika Hospitali na vituo vya Afya wanategemea  hifadhi na kinga ya wauguzi kabla ya kuonana na daktari na kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ambayo yanahitaji kutafutiwa ufumbuzi na Baraza hilo.
Mrajisi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Haji  Haji Khamis akieleza mchakato wa kulisajili Baraza la Wauguzi na Wakunga  katika uzinduzi rasmi uliofanyika Chuo cha Sayansi ya Afya Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 

 Baadhi ya washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar kwenye sherehe za uzinduzi wa Baraza hilo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments

Powered by Blogger.