VIONGOZI WA JAMII YA KIMASAI WARIDHIA KUACHA UKEKETAJI
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (kushoto) akimpongeza Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika
Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli kwenye semina ya viongozi mbalimbali
wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari
Wilayani Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa
jamii wilaya ya Ngorongoro.
Susana Koillah, Mama Shughuli na
mtafsiri wa lugha ya Kimasai katika semina hiyo akimsikiliza kwa makini
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) kabla ya kutafsiri mada
yake kwa wanasemina.
Sehemu ya washiriki wa semina ya
viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na
sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii
wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Ofisa HIV na Elimu ya Afya Taifa
wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini
Tanzania, Mathias Herman (kushoto) akitoa maelekezo kwa wana semina ya
viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi shule za sekondari, wakuu
wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro
wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Ngorongoro juzi.
Sehemu ya washiriki wa semina ya
viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na
sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii
wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
………………………………………………
VIONGOZI wakuu wa jamii ya Kimasai
wa Afrika Mashariki wameridhia kuachana na mila potofu zimezopitwa na
wakati ikiwemo vitendo vya ukeketaji kwa wasichana wa jamii ya kimasai
ambavyo vimekuwa vikiwaathiri wasichana hao kwa kiasi kikubwa.
Kauli ya kusitisha vitendo hivyo
ilitolewa juzi Wilayani Ngorongoro na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai
Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na msaidizi wake kutoka
Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni walipokuwa katika semina ya elimu ya
afya ya uzazi, kupinga vitendo vya ukeketaji pamoja na mimba za utotoni.
Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai
Afrika Mashariki, Olaiboni Simeli alimueleza Mkuu wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) na Mwakilishi wa
Shirika hilo Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues kuwa jamii hiyo ya wamasai
imeridhia kuacha mila zilizopitwa na wakati na itaendelea kushiriki
kuelimisha jamii yao zaidi juu ya madhara ya mila hizo potofu ikiwemo
ukeketaji na ndoa za utotoni.
“…Tunaishukuru UNESCO kwa
kuendelea kutoa elimu hii kwetu juu ya mila potofu nasisi tunaungana
nanyi kuendelea kutoa elimu kwa jamii yetu kupinga ukeketaji na ndoa za
utoto tumeelezwa athari nyingi zinazowapata wasichana
wanaokeketwa…kwanini tuendelee na mila zinazoleta madhara kwa watu wetu?
Tushirikiane kupiga vita hivi,” alisema Olaiboni Simeli akizungumza
mbele ya Bi. Rodrigues.
Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa
Jamii ya Wamasai Tanzania, Naimado Olaiboni alisema hakuna haja ya jamii
ya kimasai kuendelea na mila zilizopitwa na wakati ilhali mila hizo
zikiendelea kuwaathiri wamasai na kuwabakiza nyuma kimaendeleo katika
nyanja mbalimbali.
“…Tutaendelea kushirikiana nanyi kupinga ndoa za
utotoni kwa kuwa tumeelezwa madhara yake na wataalamu leo,” alisema
Naimado Olaiboni.
Naye Mkuu wa Shirika la UNESCO na
Ofisa Mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania, Bi. Rodrigues alisema
anapenda kuona Jamii ya Kimasai inaendeleza mila na tamaduni zao lakini
zile nzuri ambazo hazina chembe ya kiunyanyasaji kwa makundi yote.
Alisema ukeketaji kwa wasichanga unamadhara makubwa kwa jamii hiyo hivyo
haina budi mila hizo kupuuzwa ili kumlinda mtoto wa kike na madhara
yanayomkumba anapofanyiwa vitendo hivyo.
“…Napenda kuona Wamasai
wanaendeleza mila na tamaduni zao lakini ziwe nzuri na zisizo na chembe
ya ukatili wala unyanyasaji, tuangalie ni namna gani tunaziendeleza na
kubaki katika uhalisia wetu…nawahakikishia tutashirikiana kuhakikisha
hili linafanikiwa kwenu,” alisema Bi. Rodrigues akizungumza katika
semina hiyo.
Aidha aliwashauri jamii ya Kimasai
kupunguza kuwa na idadi kubwa ya watoto na wake ilhali mume akishindwa
kuihudumia familia hiyo jambo ambalo limeendelea kuchochea umaskini wa
familia hizo vijijini kwani watoto wamekosa mahitaji ya msingi katika
familia na kujikuta wakiishi kwa taabu.
Aliwataka Wamasai pia kupinga ndoa
za utotoni kwani mabinti wadogo wanapoolewa wanakosa fursa ya elimu
pamoja na kuunda familia bora kutokana na uduni wao katika masuala ya
afya ya uzazi kiujumla na madhara yanayowaandama katika maisha yao.
“…Ndoa za utotoni nazo ni tatizo katika jamii yetu, tuzipige vita maana
mtoto mdogo anapoolewa haweza kuunda familia bora na wala uzazi wake
hauwezi kuwa bora…,” aliongeza Bi. Rodrigues.
Zaidi ya wanasemina 210 kutoka
Kata za Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili, Aoliani Magaidulu
wakiwemo viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa
shule za msingi na sekondari na wakuu wa idara ya afya na vitengo vya
ustawi wa jamii Wilayani Ngorongoro wamenufaika na semina hiyo ya
jitihada za kuelimisha jamii juu ya mila na desturi zilizopitwa na
wakati.
Kutoka kushoto ni Mshauri na
Mkufunzi wa Masuala ya Vyombo vya Habari Jamii kutoka UNESCO Tanzania,
Rose Haji pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakifuatilia
semina hiyo iliyoandaliwa na UNESCO juzi.
Baadhi ya washiriki wa semina ya
viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za
msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa
jamii wilayani Ngorongoro wakifuatilia mada kwenye semina hiyo.
Kulia ni Mkuu wa Shule ya
Sekondari Emanyata Ololosokwani na Mwenyekiti warsha hiyo, Ole Daniel
akitafsiri kwa lugha ya kimasai mada ya Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (kushoto) alipokuwa akiwasilisha.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (kushoto) akimsikiliza Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai
Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli (kulia) kwenye semina ya
viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za
msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya na
vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya Ngorongoro.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii
ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa
idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) wakichangia mada mbalimbali.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii
ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa
idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Susana Koillah, Mama Shughuli na
mtafsiri wa lugha ya Kimasai katika semina hiyo akisisitiza jambo. Kulia
ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO)
nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira
Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii
ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa
idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Sehemu ya washiriki wa semina ya
viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na
sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii
wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai
Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni (kushoto) akichangia mada katika
semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa
shule za msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya
na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya Ngorongoro. Wengine ni
wasaidizi wa Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo
Olaiboni Simeli wakishiriki semina hiyo.
Baadhi ya maofisa kutoka Shirika
la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania
wakiwapongeza viongozi wa jamii ya kimasai, Kiongozi Mkuu wa Jamii ya
Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na Kiongozi
Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni mara baada ya
semina kumalizika.
Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai
Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na Kiongozi Mkuu wa
Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni wakipiga picha za
kumbukumbu na baadhi ya maofisa kutoka Shirika la Kimataifa la Sayansi,
Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania baada ya semina kumalizika.
Kulia ni Ofisa Mradi Elimu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na
Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Jennifer Kotta akijiandaa
kuwapongeza viongozi wakuu wa jamii ya kimasai Afrika Mashariki na
Tanzania walioshiriki semina hiyo.
Ofisa HIV na Elimu ya Afya Taifa
wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini
Tanzania, Mathias Herman (kulia) akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Jamii
ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni (kushoto) mara baada ya
semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, wakuu shule za
sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii
wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com, Ngorongoro
Post a Comment