HABARI ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania – TFF, Jamal Malinzi leo
ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
mholanzi Mart Nooij.
Akiongea na waandishi wa habari
leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema wameamua kuagana nae mbele
ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia wakati wa utambulisho wake
wakati wa kuanza kazi.
“Mpira wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari
ndefu katika mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la
vijana, sababu ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema
Malinzi.
Duniani kote chimbuko la timu
bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na vijana wengi walioanza
kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri wa kuchezea timu ya
Taifa tutakua na kikosi bora.
Nchi za wenzetu inapofikia kocha
kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na wigo mpana, kwetu sisi
wachezaji wanocheza soka nje ya nchi wanahesabika, hivyo ni lazima
tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana.
TFF ilishaanza mkakati huo ndio
maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua zikiingia kambini na kucheza
michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya
kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana mwaka 2016.
Kikosi cha U15 kinatarajiwa
kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia,
Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani mwezi April 2016
kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza michezo ya kirafiki.
Naye Mart Nooij aliyekua kocha wa
Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa habari alisema anawashukuru
watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini na TFF kwa
sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa.
Nooij alisema alifurahia maisha
yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote alichokua akifundisha timu ya
Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho wa ajira yake hana jinsi
anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka Tanzania na watanzania wote kila
siku kwa ukarimu wao.
Wakati huo huo Rais wa TFF. Jamal
Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars
akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa ambaye ni kocha wa Yanga na
Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu
ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na
AFCON.
Malinzi amesema uteuzi wa makocha
hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na
leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine
duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha hao wazawa wamekizi.
Kocha Mkwasa atakua akipewa
hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha
aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la
kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania
kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi”
Aidha Kamati ya utendaji ya TFF
Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la
uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na
timu ya Taifa.
U15 YAINGIA KAMBINI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya
Tanzania, imeingia kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa
Karume kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa
Mbeya siku ya jumapili.
Kikosi hicho kilicho chini ya
makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza mchezo huo kwa lengo la
waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na kuwaongeza wengine
watakaoneka katika kikosi hicho.
U15 ni mpango wa TFF kuandaa
kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania kufuzu ka fainali za vijana
Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar, ambapo vijana hao
watakua na umri wa miaka 16 kufikia mwakani wakati michezo ya kuwania
kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.
Post a Comment