MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD, ATEMBELEA WAGONJWA MKOA WA KUSINI UNGUJA
Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ziara ya
kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya waumini
wa Kiislamu walijumuika katika futari ya pamoja iliandaliwa na Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni.
Na: Hassan
Hamad, OMKR.
Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amefanya ziara ya kuwatembelea
na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika ziara hiyo
Maalim Seif amewaombea wagonjwa hao kuweza kupona haraka, ili waweze kuungana na
wananchi wengine katika shughuli za kimaisha, sambamba na kuwataka wale
waliofiwa kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Miongoni mwa vijiji
alivyotembelea katika mkoa huo ni pamoja na Muyuni, Kizimkazi, Kajengwa, Uroa,
Binguni na Kiboje.
Hii ni ziara yake ya
kwanza ya kutembelea wagonjwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, katika
utaratibu wake wa kutembelea wagonjwa na wafiwa kila ifikapo mwezi wa Ramadhan, ziara ambazo huzifanya
katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Wakati huo huo Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amejumuika na wananchi mbali mbali katika futari
ya pamoja nyumbani kwake Mbweni, aliyoiandaa kwa ajili ya watendaji wa vyama
vya siasa.
Amewashukuru wananchi
hao kwa kuamua kushirikiana nae katika futari hiyo, jambo ambalo amesema linaonesha
mapenzi na mshikamano miongoni kwa waislamu.
Maalim
Seif ametoa wito kwa waislamu nchini kuendeleza utamaduni wa kualikana na
kufutari kwa pamoja, kitendo ambacho hukuza na kuendeleza umoja na maelewano
kwa wananchi.
Post a Comment