Header Ads

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM, NDANI YA JIMBO LA SUMVE WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo juu ya usindikaji wa alizeti kwenye kikundi cha ujasiriamali cha KIBUKU kilichopo kata ya Lyoma ,jimbo la Sumve wilaya ya Kwimba.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kata ya Lyoma mara baada ya kujionea maendeleo ya kikundi cha Ujasiriamali kinachojishughulisha na usindikaji wa alizeti.

 Wananchi wa Kata ya malya wakionyesha Bango kubwa lenye ujumbe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana lenye madai ya kudhulumiwa viwanja ambavyo tangia walipie miaka mitatu sasa hawajapata viwanja.

Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero zao.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungunza na wakazi wa kata ya Malya ambao wanadai viwanja vyao walivyovilipia miaka mitatu iliyopita.

 Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Mganga Ndasa akiwasalimu wakazi wa kata ya Nyambiti ambao walijitokeza kwa wingi kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya CCM Kata.

Kata ya Nyambiti imetekeleza ilani ya uchaguzi kwa kiwango kiikubwa ,ina vijiji vitano na shule za msingi zimejengwa katika kila kijiji, ina zahanati katika kila kijiji, Maji yanapatikana kwa kuuzwa ndoo moja shilingi 20.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Nyambiti.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa mkutano wa Jimbo la Sumve uliofanyika Nyambiti wilayani Kwimba.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa ngoma za jadi katika kijiji cha Mwabilanda wilayani Kwimba.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Pili Moshi  katika kijiji cha Mwabilanda ambapo Katibu Mkuu alizindua mradi wa maji kwa wananchi wa kijiji cha Mwabilanda,Kwimba.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mwabilanda wakati wa sherehe za kuzindua huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji hicho.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Coretha Kulwa mkazi wa kijiji cha Mwabilanda mara baada ya kuzindua huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji hicho.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia sehemu ya kunyweshea maji mifugo katika kijiji cha Kishilili, ambapo Ng'ombe zaidi ya 800 hupata huduma ya maji safi na salama katika mradi ambao pia husaidia kaya 102 kupata maji safi na salama katika kisima kinachotumia mfumo wa jua (solar power)

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwashilalage wakati wa kuona na kushiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji.Wengine kwenye picha ni Diwani wa kata ya Sumve Ndugu Gervas Kitwala(katikati) na Mwenyekiti wa Kijiji Mzee Joseph George.

Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara mkoani Mwanza yenye lengo la kukagua,kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanganya zege wakati wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mwashilalage.

 Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Mganga Ndasa akibeba zege wakati wa kushiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mwashilalage.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wakazi wa Sumve wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano Sumve wilayani Kwimba.

 Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Pili Moshi akiwasalimia wakazi wa Sumve waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM.

 Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Ndasa akiwasalimu wakazi wa Sumve waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Mbunge wa Jimbo la Sumve akiwahutubia wakazi wa Sumve ambapo alielezea mafanikio katika kipindi chake cha uongozi ikiwa na kuwa na shule 17 za sekondari  na nyumba za walimu zote zikiwa na umeme.

 Zahanati zote jimbo la Sumve zina Umeme lakini pia alizungumzia moja ya matatizo yanayowaumiza wananchi wake ni bei ya zao la Pamba kuwa chini.

 Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu akihutubia wakazi wa Sumve kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Sumve ambapo aliwahakikishia ahadi za CCM zitatekelezwa.

 Vijana 20 kutoka Sumve wakionyesha kadi zao za Chadema kabla ya kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za Chadema kutoka kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya zaidi ya 1520 walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Sumve.

Katika ziara yake kwenye jimbo la Sumve Katibu Mkuu wa CCM amepokea kadi 48 kutoka Chadema ikiwa 28 zilizorudishwa katika kijiji cha Goloma kata ya Mwadu.

 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ukiondoka Sumve kuelekea wilaya ya Magu.

No comments

Powered by Blogger.