MAMIA WAJITOKEZA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM KUMUAGA MHARIRI EDSON KAMUKARA
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya kuagwa, Kamukara alifariki dunia juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilibrod Slaa kwenye uagaji wa mwili wa Edson Kamukara. Kulia ni Mbunge wa Bukoba mjini, Khamis Kagasheki.
Mmoja wa waandishi wa habari akiwa amepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo.
Wanahabari na waombolezaji wengine wakiwa wamejipanga foleni wakati wa utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea (katikati), akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Wanahabari ni huzuni na vilio.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki wakati wa kuuaga mwili wa Edoson Kamukara.
Wanafamilia ya marehemu wakiwa kwenye shughuli hiyo.
Sehemu ya umati wa watu katika shughuli hiyo.
Mwakilishi wa wanafunzi waliosoma na marehemu Shule ya Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi akizungumza kabla ya kutoa rambirambi yao ya sh.500,000.
Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika uagaji wa mwili wa marehemu ambapo alipigania waajiri wa vyombo vya habari kutoa mikataba ya ajira kwa wanahabari.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi akimfariji Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea alikuwa akifanyakazi marehemu Edson Kamukara.
Ni vilio tu kwa wanahabari.
Shughuli ya uagaji ikiendelea.
Dada ya marehemu Edson Kamukara akitoa heshima za mwisho.
Post a Comment