CHAMA CHA WASAMBAZAJI WA FILAMU WAFIKIA MUAFAKA
Baadhi ya wadau wa filamu nchini
ambao ni TRA, Bodi ya Filamu Tanzania na Chama cha Wasambazaji wa Filamu
wakiwa katika kikao ili kujadili changamoto katika tasninia hiyo mapema
juzi jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija, WHVUM.
Afisa Utafiti Mwandamizi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Ephraim Mdee akifafanua jambo
wakati wa kikao na wawakilishi wa Chama cha Usambazaji wa Filamu nchini
TAFDA walipokutana hivi karibuni ili kujadili changamoto zitokanazo na
ueneaji wa Filamu kutoka nje ya nchini.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Wasambazaji wa Filamu Tanzania Bw. Emmanuel Myamba (Pastor Myamba).
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akisisitiza jambo wakati wa kikao na
wawakilishi wa Chama cha Usambazaji wa Filamu nchini TAFDA walipokutana
hivi karibuni ili kujadili changamoto zitokanazo na ueneaji wa Filamu
kutoka nje ya nchini.
Katika kikao hicho Serikali na wadau hao walifikia
muafaka wakushirikiana kwa pamoja ili kuongeza kasi ya kukabiliana na
maharamia ya kazi za filamu nchini.Kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba na kushoto ni Afisa Utafiti
Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Ephraim Mdee.
Mmoja wa wajumbe wa Chama cha
Wasambazaji wa Filamu Tanzania TAFDA Bw. Suleiman Ling’ande (katikati)
akichangia mada wakati wa kikao na wawakilishi wa Chama cha Usambazaji
wa Filamu nchini TAFDA walipokutana hivi karibuni ili kujadili
changamoto zitokanazo na ueneaji wa Filamu kutoka nje ya nchini.
Post a Comment