CHANJO YA WATOTO YAZINDULIWA WILAYANI NGARA
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Chanjo ya watoto
kuzuia maambukizi ya magonjwa katika kata ya Nyakisasa kijiji cha
Kashinga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ngara mkoani Kagera
lengo la ziara hiyo likiwani ni kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi
ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana
anaongozana na Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa CCM kutoka mkoa wa
Kagera.
Wanaoshuhudia
tukio hili nyuma ni Mh. John Mongela Mkuu wa mkoa wa Kagera na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Mama Costansia Buhie.
Wakati
huo huo Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini
Ngara amesema Mamlaka ya Mapato TRA na Kikosi cha Usalama barabarani
wana kila sababu ya kupeleka huduma zao utoaji wa leseni za udereva na
huduma za usajiri wa vyombo vya moto mikoani na wilayani kwani ni
usumbufu mkubwa wanaopata wananchi kufuata huduma hizo za Leseni za
kuendesha vyombo vya moto na usajiri wa vyombo hivyo.
Amezitaka
taasisi hizo kufanya hivyo ili kuwaondolea wananchi usumbufu wanaoupata
wanapohitaji huduma hizo kutokana na umbali, Wananchi wa Ngara
wanalazimika kufuata huduma hiyo Bukoba mjini jambo ambalo linawaletea
wananchi hao usumbufu mkubwa na upotevu wa fedha bila sababu ya
msingi.
Baadhi ya akina mama na watoto wao wakisubiri watoto wao kupatiwa chanjo katika zahanati ya kijiji chaKashinga wilayani Ngara.
Mh. John Mongela Mkuu wa mkoa wa Kagera akiungumza jambo huku Nape Nnauye akimsikiliza.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Kagera Mama Costansia Buhie wakati alipokuwa akimkaribisha ili
kuzungumza na wananchi katika zahanati ya Kashinga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi hawapo
pichani wakati alipozindua chanjo ya watoto katika zahanati ya Kashinga
akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Ngara leo wa tatu kutoka kulia ni
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na katikati ni Mkuu wa
mkoa wa Kagera Mh. John Mongella
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika zahanati hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wa CCM wilayani Ngara
wakishiriki kwa pamoja katika ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Munjebwe
Rulenge.
Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika soko la Rulenge leo wakati Kinana alipofanya ziara ya kikazi katika kata hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Rulenge.
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi mbalimbali za
waliokuwa wanachama wa Chama cha CHADEMA mara baada ya kurejesha kwake
na kujiunga na CCM katika mji wa Rulenge.
Baadhi ya kadi zilizorejeshwa kwa Kinana na wananchi hao na kujiunga na CCM.
Kwaya
ya akina mama wa Rulenge wakiimba wimbo maalum wakati wa mkutano wa
hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano
wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mzee Dodwin Magambo wakati alipowasilisha malalamiko yake kwake.
Mtambo wa umeme vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua Mtambo wa umeme vijijini
REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mhandisi wa kampuni
ya kichina ya TKPE Bw.Ton Minyang wakati alipokagua ujenzi wa Mtambo
wa umeme vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya
Kabanga
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua kkikundi cha akina mama
wajasiriamali cha mjini Ngara kabla ya kuhutubia mkutano wake na
wananchi mjini humo leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata keki kuashiria uzinduzi wa kikundi hicho cha akina mama wajasiriamali.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wakati
alipokuwa akiwasili katika mkutano wa hadhara mjini Ngara leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinan akiangalia vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika mkutano huo.
MNEC
wa wilaya ya Ngara Bw. Issa Samma akizungumza na wananchi wa mjini
Ngara wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana.
Nape
Nnauye akimwaga sumu kwa wana Ngara na kuwaambia waitunze amani
waliyonayo kwani wao wanajua machungu ya amani kuvurugika katika nchi
kutokana na uzoefu wao wa kupokea wakimbizi kutoka nchi mbalimbali
jirani.
Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Ngara.
Umati wa wananchi ukisikiliza hotuba za viongozi mbalimbali waliohutubia katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Ngara akizungumza jambo na wananchi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinan akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ngara leo
Post a Comment