Header Ads

KATIBU MKUU WA CCM, KOMREDI KINANA AANZA ZIARA YA SIKU 10 JIJINI MWANZA

  • Afanya ziara jimbo la Buchosa
  • Atembelea miradi na kufanya mikutano ya hadhara
  • Asisitiza huduma za msingi zisogezwe karibu na wananchi
  • Nape awataka vijana kustuka na kutopoteza muda wao kwa vyama ambavyo vinakufa kisiasa kila kukicha.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Buchosa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk. Charles Tzeba wakati wa mapokezi Nyamadoke, wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Katibu Mkuu wa CCM amewasili Mwanza kwa ziara yenye lengo la kujenga na kuimarisha Chama ikiwa pamoja na Kusimamia, Kuhimiza na Kukagua Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Sengerema Ndugu William Ngeleja wakati wa mapokezi Nyamadoke,Sengerema mkoani Mwanza.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu wakati wa mapokezi katika kata ya Nyamidoke,ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Mwanza.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea heshima kutoka kwa vijana wa Chipukizi wa CCM mara baada ya kuwasili Nyamidoke,Jimbo la Buchosa, wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa kata ya Nyamidoke,wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na msafara wake.

 Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Zainabu R. Telack akiwasalimu wakazi wa kata ya Nyamidoke wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo akiwasalimu wakazi wa Nyamidoke waliojitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Mbunge wa Jimbo la Buchosa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk. Charles Tzeba akiwasalimu wakazi wa kata ya Nyamidoke wakati wa Mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM nkoa kwenye mapokezi yaliyofanyika kata ya Nyamidoke.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa kata ya Nyamidoke waliojitokeza kwa wingi kuja kumpokea.

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Bupandwa ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Mwanza.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM Tawi la Katwe.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua na kupokea maelezo ya ujenzi wa jengo la hospitali ya wilaya lililopo Isaka,kata ya Nyehunge.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Rumeya mara baada ya kutembelea chanzo cha maji.

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Magessa Mulongo akiwasalimu wakazi Nyakaliro,kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

Mkuu wa Mkoa alisema ,Serikali jijini Mwanza imesisitiza iko makini kwenye usimamizi wa zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la wapiga kura kupitia mfumo wa kielectronic wa BVR kwenye wilaya mbalimbali za mkoa huo. 

Zaidi ya wananchi 57000 wamejiandikisha kwenye daftari hilo ndani ya wiki mbili wilayani Sengerema.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Nyakaliro ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Mwanza.

 Wananchi wa kata ya Bukokwa wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Buchosa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk. Charles Tizeba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Bukokwa wilaya ya Sengerema.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria kuzindua huduma ya maji safi na salama kwa wakazi kata ya Kalebezo.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kata ya Kalebezo kama ishara ya kuzinduliwa rasmi huduma ya maji.

 Mbunge wa Jimbo la Buchosa ambaye pia ni Naibu Waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizeba akihutubia wakazi wa kata ya Nyahunge ambapo aliwaambia wananchi hao, utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye Jimbo la Buchosa katika sekta zote na huduma za jamii.

 Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu akiwasalimu wakazi wa Nyehunge kabla ya kumkaribisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuhutubia.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyehunge ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyehunge ambapo aliwasihi vijana kuacha kufuata vyama vinavyopoteza muda wao kwani hivyo vyama havina sera mbadala wa kuleta maendeleo.

 Wananchi wakisikiliza hotuba za viongozi wa CCM Kitaifa.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyehunge wilaya ya Sengerema ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Mwanza.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Nyehunge, Sengerema mkoani Mwanza ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa atazungumza na wabunge wa CCM kwenye Bunge lijalo wabadili sheria zinazokandamiza wananchi.

 Wakazi wa kata ya Nyehunge wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Mwanza.

(Picha zote na Adam Mzee)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments

Powered by Blogger.