Header Ads

KAMPUNI YA HUAWEI TANZANIA NA WIZARA YA MAWASILIANO WAUNGANA KATIKA KONGAMANO LA TEKNOHAMA

Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Bwana Samson Majwala katika ushirikiano wao huo. anayefuatia ni Afisa wa Huawei. 

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Huawei Tanzainia ikishirikiana na Wizara na Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inatarajiwa kufanya kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference katika ukumbi wa Julius Nyerere Convential Centre (JNICC)  kwa siku mbili yaani Juni 18 na 19  mwaka huu.
Kongamano hilo litajadili hali ya sekta ya Teknohama kwa sasa, sera mpya zitakazo wekwa na kuweka ajenda ya jinsi ya kukuza sekta hiyo nchini. Pia kongamano hilo litaainisha jinsi nchi itafikia malengo yake milenia kupitia teknohama.
Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba alisema, “Tumefurahi sana kwamba wizara na Kampuni ya Huawei Tanzania zitashirikiana katika kongamano hilo, ambapo tutajadiliano kwa undani ukuaji na maendeleo katika sekta ya ICT, Na kwa upande wa wizara tutaelezea sera mpya na mipango tuliyoweka ilikuhakikisha maendeleo ya sekta”.
Aliendea kwa kuwahakikishia watanzania kwamba wizara imejikita katika kukuza sketa ya Teknohama. Aliongeza kwamba Makamu wa Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania anategemewa kuwa mgeni rasmi, huku pia Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Balozi wa China nchini Tanzania watakuwepo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Bwana Samson Majwala alisema, “ Tunaishukuru sana wizara kwa kukubali kuungana nasi katika kuaanda kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference nchini Tanzania, na tunawahakikishia watanazania wote kwamba kongamano litapendeza. 

Tutakuwa na wataalamu kutoka nyaja tofauti za Teknohama kutoka serekalini na Kampuni ya Huawei ambao watatuelimisha kuhusu mitindo mipya katika sekta hiyo. Sisi kama Huawei tutaelezea mipango tuliyonayo ya kuboresha sketa hii nchini Tanzania”.
Katika kongamano hilo, Huawei watazindua bidhaa zao mpya za Oceanstor V3 na Fusioncube. Pia kutakuwa na gari maalum ya kufanya maonyesho, gari hilo kwa kila mwaka linafanya ziara katika mabara yote duniani, na kwa mwaka wa 2015 litazuru bara la Afirka haswa Afrika Kusini na Afrika Mashariki, Tanzania ikiwemo moja ya nchi itakayo pita.

No comments

Powered by Blogger.