Header Ads

KATIBU MKUU WA CCM, NDG KINANA ATEMBELEA SOKO LA MJINI SENGEREMA LEO ASUBUHI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabishara wa Soko Kuu Sengerema mjini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia miundo mbinu ya maji taka inayolalamikiwa na wafanyabiashara wa soko kuu la Sengerema.

Na Mwandishi wetu - Sengerema 

  Wafanyabiashara wa Soko Kuu Sengerema mjini wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo baada ya kuwanyimannafasi ya kuendeleza eneo la Soko. 

Wakizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ),  Abdulrahman Kinana kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wamelalamika kukosekana kwa maji safi na salama,miundo mbinu mibovu ya maji taka pamoja na vyoo .


Pia walilamikia kunyimwa nafasi ya kujenga vibanda vya biashara kwa madai Halmashauri inataka kujenga soko la kisasa ambalo limekuwa ahadi kwa zaidi ya miaka 10 sasa.

 Wamesema wanashangaa uongozi unawanyima nafasi ya kujenga lakini viongozi haohao wanashindwa kujenga kwa madai ya kukosa fedha huku wakiendelea kukusanya ushuru kila kukicha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments

Powered by Blogger.