Header Ads

CHINA YAVUTIWA NA ENEO LA VIWANDA WILAYANI KISARAWE MKOANI PWANI

 Kibao kinacho elekeza eneo la mradi wa viwanda wilayani Kisarawe mkoani Pwani lililopo Visegese. Mradi huo unaendeshwa na Halmshauri hiyo na wabia wa Kampuni ya World Map.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro (kushoto), akizungumza na viongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe,  Wabia wa eneo la mradi wa Kampuni ya World Map  na wawekezaji kutoka nchini China waliofika wilayani humo jana kuangalia fursa za kuwekeza viwanda katika eneo hilo. Kulia ni Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily.
 Wawekezaji kutoka China wakiwa katika mkutano na uongozi wa wilaya ya Kisarawe na wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map kabla ya kwenda kuona eneo la mradi wa viwanda. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Makampuni ya Huallan 'Huallan Group', Tu Huobao, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo, Apple Ye, Huang Haitao na Meneja Masoko, Nara Zhou.
 Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wawekezaji hao. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro,  Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Kigalu, Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng'imba.
 Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Adam Ng'imba (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko na Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Kigalu.
 Mkuu wa Wilaya hiyo, Subira Kigalu akizungumza katika mkutano huo.
 Wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map na viongozi wa idara mbalimbali za wilaya hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wakuu wa idara wa wilaya ya Kisarawe wakiwa kwenye 
mkutano huo.
 Mkutano na wawekezaji ukiendelea.
 Maofisa wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map wakiwa kwenye mkutano huo.
 Miundombinu ya barabara inavyoonekana eneo la mradi.
 Katapila likiwa eneo la mradi kutengeneza miundombinu ya barabara.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Brendan Maro (katikati), akiwaonyesha ramani ya eneo la mradi wawekezaji hao. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng'imba.
 Mazungumzo eneo la mradi.
 Sehemu ya eneo la mradi.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Subira Kigalu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji hao na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map.

Na Dotto Mwaibale 

KATIKA  kukuza uchumi kwa wakazi Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani mradi wa uendelezaji wa viwanja katika mji mdogo wa Kisarawe  uliopo Kijiji cha visegese umeanza kupata wawekezaji kutoka nchini China ili kusaidia kuendelea wilaya hiyo kwa kujenga viwanda.

Wilaya hiyo  kwa kushirikiana na wabia kutoka kampuni ya world Map   wameweza kupima viwanja zaidi ya 250 katika kijiji hicho kwa ajili ya viwanda  na Kutangazwa katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), na hatimaye kuanza kupata wawekezaji ambao wametemebea katika wilaya hiyo na  kujionea maeneo ya viwanda hivyo.

Awali kabla ya kutembea katika Kijiji cha visegese ambapo kuna viwanja  ya maeneo ya uwekezaji mkuu wa wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu  ambaye ni mwenyeketi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo aliwakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikisha mazingira ya usalama  kwa ajili  uwekezaji

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoka  amekishukuru kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kuwaleta wawekeza hao ili kufanikisha wananchi wa wilaya hiyo wanakuwa na uchumi wa kati na kuongeza kodi kwa serikali.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Brendan Maro alisema wilaya hiyo imepiga hatua katika kutenga maeneo ya viwanja kwa ajili ya uwekezaji hivyo kwa sasa kituo hicho hakinabudi kupeleka wawekezaji katika maeneo ya pembezo.

Katika mradi huo wa viwanja 291 ambao asilimi 63 ni kwa ajili ya wananchi na asiliami 37 ni kwa ajili ya halamshauri ya wilaya ya Kisarawe na wabia wa mnradi huo  kwa mafanikio hayo uwe ni chachu kwa halmashuri zingine ili kukuza uchumi kwa wananchi kwa kutenga maeneo ya viwanda na kupima hali itakayosaidia kuepukana na mipango miji holela.

No comments

Powered by Blogger.