KATIBU MKUU WA CCM NDG ABDULRAHMAN KINANA, AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WACHIMBAJI WADOGO WILAYANI BUSANDA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katoro mkoani Geita ambapo aliwaambia wananchi hao mwekezaji mzuri nchi wa kwanza ni mwananchi mwenyewe, pia alizungumzia sheria ambazo nyingi zinazowakadamiza wananchi,zinapoteza nguvu kazi,zinawanyima haki wachimbaji wadogo zapaswa kufutwa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Katoro waliojitokeza kwa wingi ,Katika mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaambia wakazi hao vyama vingi vya siasa vimeshindwa kuendelea kutokana na kukosa sera,kushindwa kusimamia mambo pamoja na kuwa na viongozi wasiokubali mabadiliko na kung'ang'ania madaraka.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa somo la siasa kwa wakazi wa Kata ya Katoro.
Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhe.Mh Lolensia Bukwimba akihutubia wakazi wa Katoro kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisoma bango la kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Wananchi wa kata ya Katoro wakishangilia ujio wa Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara Katoro.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Na Mwandishi wetu - Geita

Hakuna ubishi kwamba Sekta ya madini ni eneo pekee kama
likitumika vizuri linaweza kuchangia ukuaji wa uchumi kwa nchi ambazo zinapiga
hatua kwenye suala la maendeleo Barani Afrika.
Tanzania licha ya kuwa na rasilimali hiyo kwenye mikoa ya
MANYARA na SHINYANGA wananchi wake bado wanaishi kwenye hali ya umasikini huku sababu
ikielezwa, Serikali kwa kushirikiana na wawekezaji wa kigeni wameamua kuihodhi ardhi
yenye madini ikiwasahau wazawa.
Changamoto hiyo haiishii mikoa hiyo miwili, kwani jamii
ya wachimbaji wadogo wa madini wilayani BUSANDA mkoani GEITA, wanalishutumu
Shirika la madini la taifa STAMICO,
kwa kitendo cha kuwafurusha kutoka maeneo ya uchimbaji kwenye mgodi wa
NYARUGUSU licha ya agizo la Rais JAKAYA KIKWETE.
Baada ya kusikiliza maelezo ya wachimbaji hao wadogo,
kisha katibu mkuu huyo wa chama chama mapinduzi CCM, komredi KINANA akaahidi
kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mji wa KATORO wilayani humo,
kulimaliza suala hilo ndani ya mwezi mmoja.
Madai ya wachimbaji wadogo wa madini mkoani humo yamekuwa
ya muda mrefu, suala kubwa wanalohitaji kutoka Serikalini iwaruhusu kuendelea
na shughuli zao za utafutaji wa madini kwenye machimbo ya NYARUGUSU,
MWANHALANGA na NYALUYEYE ili kuinua hali za vipato vyao.
Post a Comment