Naibu Waziri wa Afya, Dkt Hamis Kigwangalla akikagua Bidhaa Feki akiwa pamoja na maofisa wengine wa Serikali katika Msako huo uliofanyika eneo la Sinza Jijini Dar es Salaam na Kubaini Kiwanda feki cha Kutengeneza Pombe kali
..............................................
Naibu Waziri Wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla ameongoza kikosi kazi katika msako wa Viwanda vinavyotengeneza pombe Kali feki ikiwemo viroba na zinginezo na kufanikiwa kukamata kiwanda feki kilichopo maeneo ya sinza jijini Dar es salaam.
Akiingoza msako huo Naibu Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa msako huo unaofanywa na Wizara hiyo inashirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA umefanikiwa kukamata kiwanda feki kinachotengeneza pombe aina ya viroba, konyagi, Smirnoff na zedi kilichopo sinza jijini Dar es salaam.
"Tunafanya msako huu kwa kushirikiana na kikosi kazi cha Serikali ili kuondoa pombe haramu zinazotengenezwa kiholela na kwa kutozingatia viwango vya ubora kwa maendeleo na Afya ya watanzania" alisema Dkt. Kigwangalla.
Aidha Dkt. Kigwangalla ameongeza kuwa katika msako huo wamefanikiwa kukamata kiwanda hicho kikiwa na nyenzo za kutengenezea pombe haramu kama vile chupa za konyagi, vifuniko, lebo, vifuko na nyenzo zingine za kutengenezea pombe hiyo haramu.
Dkt. Kigwangalla amesema kuwa msako huo umebaini kwamba watengenezaji hao wanatumia gongo na spiriti kutengeneza pombe kali kitu ambacho ni hatari kwa afya ya watanzania hususani vijana hivyo kufanya nguvu ya taifa kupotea.
Katika msako huo pia ulifanikiwa kukamata maduka yanayouza pombe hizo maeneo ya Mwenge na Manzese jijini Dar es salaam ikiwa chini ya msambazaji Bw. Yusuf Yusuf Abdul Kalambo mkazi wa Kimara ambaye anatafutwa na jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Zoezi hilo la kusaka Viwanda feki vinavyotengeneza pombe kali linafanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TFDA pamoja na jeshi la polisi ni endelevu mpaka bidhaa feki zitapotoweka nchini.
|
Post a Comment