Wanaume Wakatoliki Wawatembelea Masista Wadada wadogo wa Mtakatifu FRANSISKO Mbagala
Waumini wa Kanisa Katoliki wakiandamana wakati wa kuanza ibada ya Masista wa Jimbo la Dar es Salaam wa Shirika la Dada Wadogo la Mbagala Misheni baada ya kutembelewa na Umoja wa Wanaume wa Kanisa Katoliki (Uwaka), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao jukumu lao kubwa ni kuwalea watawa hao.
Monsinyori Padri Deogratius Mbiku . wa Parokia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) (katikati), akiongoza ibada ya misa takatifu. Kushoto ni Padri Msaidizi wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph, Edward Sabbas na kulia ni Katibu wa Jimbo hilo, Aidan Mubezi.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (kulia), akishiriki sakramenti takatifu wakati wa ibada hiyo. |
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakinunua mvinyo wa Aloe vela.
Waumini wakisali mbele ya msalaba nje ya kibanda maalumu cha msalaba wa Yesu.
waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
Na Dotto Mwaibale
Watanzania
wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi na kudharau kazi zingine kwani mbele
za mungu kazi zote ni sawa na zinaheshimika.
Hayo
yameelezwa na Monsinyori Padri Deogratius Mbiku katika ibada takatifu ya
kuombea Umoja wa Wanaume Katoliki (Uwaka) kuwasaidia kwa hali na mali masista
wa Shirika la Dada Wadogo wanaoishi eneo la Mbagala Misheni jijini,
Dares Salaam.
Akitoa
mahubiri katika ibada hiyo, alisema binadamu anapenda kuchagua kazi huku
akionya kuwa watu waache kudharau kazi yoyote inayofanywa na mwingine ilimradi
iwe ya halali.
“Tusidharau
tufanye kazi na asiye fanya kazi hastahili kula. Hata familia yaYesu ililala
njaa…hata ukilala njaa usidharau kazi,”alisema.
Akimzungumzia
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, PadriMbiku alisemaalikuwa mtu wa kwanza
kuwaomba masista kuombea nchi ilipovamiwa na majeshi yaIdd Amin wa Uganda.
“Nyerere
aliwashukuru sana watawa masista kwa kushinda vita ile dhidi ya Idd Amin,
Tanzania haikuzoea vita.
“Hivyo
aliomba masista wasali sana. Tanzania ikashinda.
Nyerere
alisema waziwazi na washukuru masista kwa kushinda vita,” alisema Mbiku.
Vita kati
ya Tanzania na Uganda iliibukamwaka 1978 nakufikia tamati mwaka 1979
baadayamajeshi ya Amin kuchakazwa vibaya na Jeshi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ).
Kutokana
na umuhimu wa sala za masista hao, Padri Mbiku aliwaomba Uwaka
kuhakikisha wanawasaidia masista kwani wanamchango mkubwa kwa taifa na
kanisa.
Post a Comment