PPF yakaribishwa Kuwekeza Wilayani SAME kwenye Kiwanda cha Tangawizi
Mkuu wa Wilayaya Same, mkoani Kilimanjaro, Bi. Rosemare Staki Senyamule, (kulia), akimkaribisha ofisini kwake, Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele Oktoba 10, 2016.
Na KHALFAN SAID, SAME
MKUU
wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Rosemary Staki Semanyule, (pichani), amesema wilaya
yake inazo fursa za kutosha hususan kilimo cha Tangawizi na kuukaribisha Mfuko wa
Pensheni wa PPF kujenga kiwanda cha kuchakata Tangawizi, ili kuongeza thamani
ya zao hilo.
Mkuu
huyo wa wilaya aliyasema hayo katika mazungumzo mafupi na MenejaUhusiano wa
Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele, aliyemtembelea ofisini kwake Oktoba
10, 2016.
“Same
tunalima Tangawizi kwa wingi, wakulima hawapati faida ya kutosha kwa vile
wanauza mara tu wanapovuna, tunahitaji viwanda vya kuchakata Tangawizi ili iwe
katika mfumo wa unga (powder) na itakuwa rahisi kusafirisha nje na kuuza kwa
bei ya juu zaidi na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima wetu.” Alisema Bi Staki.
Bi.
Staki pia alisema, ukiacha wananchikujishughulisha na zao hilo, pia Same
wanalima mazao ya chakula kwa wingi.
Kwa
upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, alisema, PPF inaendelea
na kampeni yake ya kuongeza wanachama hususan kupitia mpango wa “Wote Scheme”
unamuwezesha Mfanyakazi wa sekta rasmi na isiyo rasmi, (wajasiruimali) kujiunga
nao.
“
Wote Scheme, ni mpango utakaowafaa sana wajasiriamali, ambao ni wakulima,
waendesha bodaboda, mama lishe na baba lishe.” Alisema Bi Mengele.
Akifafanua
zaidi, Bi.Mengele alisema, Mwanachamaaliyejiunga na mpango huo, atafaidika na
Mafao mbalimbali na kubwa zaidi ni kupata Bima ya Afya.
Bi. Staki akimsikiliza Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele.
Meneja Uhusiano wa PPF, Bu.Lulu Mengele, (kushoto), akimueleza Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Bi. Rosemary Staki Semanyule, shughuli mbalimbali zifanywazo na PPF hususanMpango wa Wote Scheme.
Post a Comment