Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilamba, kushoto ni Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu.
................
Naibu Waziri Ofisi
ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo
amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya ya Temeke kwa kutekeleza maagizo
yake aliyoyatoa mwezi mmoja aliopita ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi
wanakaa kwenye madawati na kuongezwa vyumba vya madarasa.
Mnamo mwezi
Septemba mwaka huu, Jafo alizitembelea shule nne za wilaya ya Temeke zilizopo
eneo la mbagala na kukutana na changamoto lukuki, zikiwemo kutotembelewa shule
hizo na Afisa elimu wilaya toka mwaka huu uanze kitendo kilicho sababisha
kutobainika kwa changamoto ili zipatiwe ufumbuzi.
Shule
alizozitembelea ni pamoja na shule za msingi Chemchem, Nzasa, Charambe, na
Kilamba ambapo Jafo alikuwakuta watoto wa darasa la saba pekee kwa shule ya
Chemchem ndio waliokuwa wakikalia madawati.
Katika shule ya
nzasa, Naibu Waziri huyo aliwakuta watoto wamejazana huku kukiwa hakuna mpango
wowote wa ujenzi wa madarasa.
Aidha
aliwakuta walimu wakiwa hawana ofisi ya walimu licha ya shule hizo kuwa katika
jiji la biashara lenye mapato mengi.
Hata hivyo, Shule
ya Kilamba pekee ndiyo ilikuwa katika hali ya kuridhisha, na baada ya ziara
hiyo alitoa maagizo kwa mkurugenzi wa Temeke kuzifanyia kazi changamoto alizo
zibaini kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Jafo alifanya
tena ziara kwenye eneo hilo ili kubaini utekelezaji wa maagizo yake na katika
safari hiyo ya pili alifanikiwa kuzitembelea shule alizozitembelea awali pamoja
na shule mbili nyingine za Kiburugwa na Kinguki.
Alipofika alikuta
watoto wote wakiwa katika madawati pamoja na kuanza kwa harakati za kuongeza madarasa
na ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule hizo ambazo baadhi zilikuwa hazina.
Kadhalika,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, alimpa taarifa Jafo kuwa shule ya nzasa
itapata jumla ya vyumba saba, Chemchem vyumba vitano, chalambe vyumba
vinne na ofisi ya walimu na kilamba kujengewa fensi ya shule.
Naibu Waziri huyo
aliwashukuru na kuwapongeza viongozi wote wa temeke kwa kujali matatizo ya
jamii.
Katika ziara hiyo
Jafo aliongozana na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Mbunge wa jimbo la Mbagala Issa
Mangungu, Meya ya Temeke Chaurembo, Mkurungenzi wa Manispaa ya temeke na
wakuu wake wa idara huku akisema viongozi hao ni mfano wa kuigwa.
|
Post a Comment