Mkutano wa Robo Mwaka Chama cha Majaji na Mahakimu Kanda ya Ziwa Wafanyika
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita, unaofanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini Mwanza.
Mongella amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa uwazi masuala ya maadili kwa watumishi wa umma na kwamba yawe ajenda ya kudumu katika ngazi mbalimbali za utendaji serikalini hususani katika ngazi ya mahakama.
Amesisitiza mkutano huo kutoka na maadhimio yanayohimiza mahakama kutenda haki na kuleta manufaa kwa wananchi na kuondokana na malalamiko kwamba mahakama hazitendi haki katika maamuzi yake.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, chama hicho kinahakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kutenda haki na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa chombo hicho katika utoaji wa haki.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.
Na BMG
Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe.Robert Makaramba, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, akizungumza na wanahabari nje ya mkutano huo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi mkoani Mwanza, Mhe.Wilbert Martin Chuma, akizungumza kwenye mkutano wa robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu mikoa ya Mwanza na Geita, unaofanyika leo Jijini Mwanza.
Post a Comment