Mbunge wa Jimbo la Chalinze RIDHIWANI KIKWETE achangia Damu
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa katika zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya Mama na mtoto, jimboni humo. |
Mbunge Ridhiwani akipimwa mapigo ya mojo kabla ya kutoa damu,upimaji wa mapigo ya moyo ni muhimu katika zoezi la utoaji damu. |
Mbunge Ridhiwani akipata maelekezo kutoka kwa wahudumu wa afya katika zoezi hilo la kuchangia damu. |
Mbunge Ridhiwani Kikwete wa katikati akiwa na Mwenyekiti wa CCM kata ya Chalinze wa kushoto Bwana Nassar Tamim na Mratibu wa zoezi hilo la uchangiaji damu Bwana Lazaro. |
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na Diwani wa kata ya Pera wa kulia,na Mwenyekiti wa wakinamama Kata ya Pera Bi.Esther Laban wakitembea kuangalia lambo la maji lililojaa matope. |
Viongozi hao wakiangalia Lambo hilo la maji. |
Mbunge wa Chalinze wa tatu toka kulia akisikiliza maelezo kutoka kwa viongozi hao hatua walizochukua baada ya lambo hilo kujaa matope. |
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akipokolewa na kinamama wa jamii ya wafugaji wa kabila la Kimaasai alipofika kuwatembelea na kuzungumza nao. |
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisikiliza mmoja wa kina mama aliyesimama kuzungumza kuhusu kero wanazopata katika shughuli zao za kifugaji . |
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji aliyesimama akizungumzia athari zizokanazo na sheria namba 10 ya mwaka 2010 katika kikao na Mbunge wa jimbo la Chalize Ridhiwani Kikwete. ................. |
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,ameshiriki
katika zoezi la kuchangia damu linalotambulika ‘’Changia Damu Salama kwa Mama
na Mtoto’’lilifanyika jimboni humo ili kusaidia upatikanaji wa damu salama.
Akizungumza katika zoezi hilo Ridhiwani amesema kuwa
amevutiwa na zoezi hilo na kuamua kujitolea kuchangia damu ili kumkomboa mama
na mtoto.
Katika tukio lingine Ridhiwani amekutana na kufanya mazungumzo na wakinamama wa jamii ya wafugaji
wa kabila la wa Maasai ili kuangalia ni namna gani atasaidia kutatua changamoto
zinazowakabili wafugaji katika jimbo hilo.
Aidha amepata nafasi ya kutembelea Lambo la maji lililojaa
matope katika eneo la Pera ili kujionea hali halisi ya eneo hilo ili kusaidia
kurudisha lambo hilo katika hali yake ya kawaida.
Post a Comment