Header Ads

Mama JANETH MAGUFULI aiomba Jamii Ijitokeze Kuwasaidia Wazee Wasiojiweza


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na viongozi wa mkoa mara baada ya kuwasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea vituo vya kulea wazee na watu wasiojiweza vya Chazi na Fungafunga vyote vilivyopo Mkoani huko.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni Ikulu Ndogo Mkoani Morogoro.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya watoto alipofika kutembelea makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.

Baadhi ya Viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro wakimuonesha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli maeneo ya miradi yaliyo katika makazi hayo.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee wanaoishi katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.

 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Regina Chonjo akiongea na wazee makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga  na kuwataka viongozi wa kituo hicho kuwasiliana mara kwa mara na viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada ili kusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.

Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akishukuru Mama Janeth Magufuli kwa uamuzi wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa wazee na watu wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli hotuba.

Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na Wazee katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro ambapo amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi ya Chakula Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph Kaniki.

Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph Kaniki. Akimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa msaada wa chakula na kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo kwani kusaidia wazee ni kulisaidia taifa pia.

.....................................


Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo.


Hayo yamesemwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati akiongea na wazee na watu wenye ulemavu alipotembelea kituo cha wazee na watu wenye mahitaji maalum cha Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.


“Kundi hili ni moja kati ya makundi yaliyokatika hatari kubwa sana na kwa kiasi kikubwa ni kundi ambalo limekuwa likisahaulika sana na kuwafanya kukosa mahitaji muhimu wanayopaswa kuyapata hivyo rai yangu kwa Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu”. Alisema Mama Janeth.


Pia Mama Janeth alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inatambua kuwa wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu.


Aidha, Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa Mchele kilo 875,Unga Kilo 875, Sukari Kilo 175, Maharage Kilo 350  na Mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi boksi 1 Mama Janeth aliwataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha chakula hicho kinawafikia walengwa kama ilivyopangwa.


Akiongea wakati akimkaribisha Mama Janeth Magufuli, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Regina Chonjo aliwataka ameataka viongozi wa kituo hicho kuwasiliana mara kwa mara na viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada ili kusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.


Naye Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo hicho Bw.Rashid Omar alimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa uamuzi wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa wazee na watu wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.


PICHA/HABARI NA HASSAN SILAYO


No comments

Powered by Blogger.