Elimu ya Mpiga Kura yawavutia Vijana Wengi Mkoani SIMIYU
Baadhi ya vijana
wakijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na Maofisa wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi –NEC (Kulia) waliokuwa wakitoa Elimu ya Mpiga Kura wakati wa
maadhimisho ya Wiki ya Vijana mkoani, wilayani Bariadi, Simiyu. Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) inaendelea kutoa Elimu ya Mpiga kura nchini kwa kukutana na
wananchi wa makundi mbalimbali.
Afisa kutoka Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Hubert Kiata akitoa elimu ya Mpiga kura kwa wakazi
wa wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
Baadhi ya wananchi wa
wilaya ya Bariadi waliojitokeza kupata Elimu ya Mpiga Kura iliyokuwa ikitolewa
na Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mkoani Simiyu. Tume ya Taifa ya
Uchaguzi imeanzisha programu endelevu za kuwafikia wananchi moja kwa moja
kuwapatia elimu ya mpiga kura kupitia mikutano, maonesho mbalimbali na vyombo
vya habari.
Maofisa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) Bw. Hurbert Kiata (kulia) na Upendo wakisikiliza kwa makini
Hoja na maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na vijana wa wilaya ya Bariadi
kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Taratibu na Sheria zinazosimia Chaguzi za
Tanzania.
Picha / Aron Msigwa –NEC.
Picha / Aron Msigwa –NEC.
Post a Comment