Mkurugenzi wa asasi ya msaada wa kisheria ya LASWA mkoa wa Iringa Francis Mwilafi akizungumza wakati wa uzinduzi wawa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria
kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama
wajawazito na watoto,warsha iliyoshirikisha madiwani na watendaji wote wa kata za wilaya ya Kilolo ,kulia ni meneja wa LASWA Oscar Lawa.
Katibu tawala wa wilaya ya Kilolo Yusuph Msawanga akizindua wa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria
kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama
wajawazito na watoto.
Madiwani wa Halmashauri ya Kilolo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katibu tawala wa Kilolo Yusuph Msawanga wa nne kutoka kulia mara baada ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria
kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama
wajawazito na watoto.
Mkurugenzi wa Laswa akieleza lengo la mradi huo.
|
Watendaji wa kata zote za Kilolo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katibu tawala wilaya ya Kilolo. |
|
Katibu tawala wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Yusuph Msawanga (wa
nne kulia waliokaa) akiwa na mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali
inayojihusisha na huduma ya msaada wa kisheria wa bure kwa wananchi
mkoani Iringa Francis Mwilafi kushoto kwake na baadhi ya wafanykazi
wa LASWA na madiwani mara baada ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha
huduma ya wasaidizi wa kisheria
kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama
wajawazito na watoto
...........................
MKUU
wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah ameiomba asasi
iyoso ya kiserikali inayojihusisha na msaada wa kisheria ya
LASWA kusaidia kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili kuwezesha
jamii wilayani humo kujua sheria na kukomesha mimba za utotoni na
unyanyasaji kwa wanawake .
Akizungumza
katika uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa
kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa
akina mama wajawazito na watoto , jana mkuu huyo aliyewakilishwa na
katibu tawala wa wilaya hiyo Yusuph Msawanga alisema kuwa mradi
kuzinduliwa kwa mradi huo katika wilaya ya Kilolo iwe ni mwisho wa
jamii kunyanyasika na iwe mwisho wa mimba za utotoni .
Alisema
kuwa jamii kutokana na kutojua sheria ama wajibu wao kwa watoto
kumekuwepo na changamoto za watoto wa kike kukatishwa masomo yao
kutokana na mimba za utotoni ama wato kuwatorosha kwenda kufanya
kazi jambo ambalo kisheria ni kosa .
Hivyo
alisema kutokana na mafunzo hayo yametolewa kwa madiwani na
watendaji wa kata zote za wilaya ya Kilolo na LASWA kutoa wasaidizi
wa kisheria kwa kila kata ni uwazi kuwa jamii itaelimishwa juu ya
sheria mbali mbali na hata kuwezesha changamoto za mimba za
utotoni na wajane kunyanyasika kwa kutojua haki zao kupungua zaidi.
"
Nawaombeni sana washiriki wa mafunzo haya ambao ni madiwani na
watendaji wa kata tumieni mafunzo haya kusaidia jamii kuepukana na
unyanyasaji wa aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupambana na
wale wanaokwamisha watoto wa kike kuendelea na masomo kwa kuwapa
mimba ....ila kwa LASWA naomba sana mzidi kutoa mafunzo haya kwa
makatibu tafara ikiwezekana hata kwa watendaji wa vijiji ili elimu
hii iwafikie watu wengi zaidi"
Kuhusu
wasaidizi wa kisheria wa LASWA waliopo katika ofisi za watendaji
ngazi ya kata alisema kuwa ni vizuri kila mmoja kufanya kazi yake
kwa kusaidia jamii na kuepuka kutumika kukandamiza watu wasiojua
sheria
Kuwa
iwapo wasaidizi hao watasaidia kutoa elimu ya msaada wa kisheria
kwa wananchi wenye uhitaji upo uwezekano mkubwa wa jamii wilayani
humo kujikita zaidi katika uzalishaji mali badala ya kupoteza pesa
nyingi kwenda kutumia katika kesi mahakamani .
Meneja wa LASWA Oscar Lawa alisema kuwa kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na asasi yake ya LASWA Iringa kwa ufadhili
wa LSF ya jijini Dar es salaam kwa chini ya ubalozi wa Denmark
kuwa sifa ya msaidizi wa kisheria ni kuwa na akili timamu pia
sifa ya kuheshimu na kulinda sheria za mbali mbali za nchi na haki
za binadamu
Mkurugenzi huyo alisema hadi sasa wamekwisha toa mafunzo na kuwa
na vijana katika wilaya zote tatu za mkoa wa Iringa ikiwemo ya
Kilolo, Mufindi na Iringa kwa kuwa na vijana wasaidizi wa kisheria
Aidha alisema faida kubwa ya msaidizi wa kisheria ni kupunguza na
kuziba pengo la ukosefu wa huduma za msaada wa kisheria katika jamii
anayoishi kwa kutoa usaidizi wa awali wa kisheria.
Hata
hivyo alisema lengo kuu la mradi huo ni kufanya wasaidizi wa
kisheria (Paralegals) kujengeka kiuwezo na wafahamike katika
jamii wanazoishi na kuwawezesha kuwafikia kiurahisi wahitaji katika
maeneo yao .
Ili
kuwezesha kufikiwa kwa lengo hili la mradi unahitaji ushirikiano
wa kutosha kutoka kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya
kitongoji hadi ngazi ya wilaya na kuwa wasaidizi hao wa kisheria
bila kupata ushirikiano kutoka kwa madiwani na viongozi wote wa
ngazi ya kijiji hadi wilaya kwani pasipo hivyo wananchi
watacheleweshwa kupata haki yao.
"Muda
wa utekelezaji wa mradi huu ni miaka minne kwa gharama ya milioni
100 ambapo vituo vya wasaidizi wa kisheria watalipiwa pango la ofisi
na kupewa nauli ya kuwafikia wahitaji wa huduma ya bure ya kisheria
maeneo mbali mbali pia kutumika kufikisha elimu ya kisheria mfano
katika mikutano ya hadhara ,mabaraza ya maendeleo ya kata kila mwaka
kituo cha msaada wa kisheria kitapewa Tsh milioni 8 za uendeshaji "
Huku
mkurugenzi mkuu wa LASWA Iringa Francis Mwilafi pamoja na
kuwapongeza washiriki wa warsha hiyo na uongozi wa wilaya ya Kilolo
kuutambua mradi huo bado alitaka viongozi wote wa serikali na
madiwani kutoa ushirikiano mkubwa kwa wasaidizi hao wa kisheria ili
kuwezesha jamii kuweza kunufaika na mradi huo .
Mwilafi
alisema kumekuwepo na mafanikio makubwa ya mradi huo kwani hadi
sasa LASWA mkoa wa Iringa imefanikiwa kuweka msaidizi wa kisheria
kwa kila kata ya wilaya zote za mkoa wa Iringa.
| |
Post a Comment