WAZIRI MEMBE ARUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS MAKAO MAKUU YA CCM MJINI DODOMA
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe
akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara,
Rajabu Ruhavi baada ya kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM,
mjini Dodoma jana kurudisha fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, baada ya kupata
wadhamini wanaohitajika.
Picha zote na John Badi
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe
(katikati), akizungumza na wanaCCM baada ya kurejesha fomu za kuomba
kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Makao
Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Dodoma jana, baada ya kupata
wadhamini wanaohitajika. Kulia ni Mkewe Mama Dorcas Membe na (kushoto)
ni Kada wa CCM, Kapteni mstaafu Alhaj Mohamed Ligola.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe
(katikati), akikabidhi fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Bara, Rajabu Luhavi alipozirejesha katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM,
mjini Dodoma jana, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. Kulia ni
Mkewe Mama Dorcas Membe.
Post a Comment