RAIS WA ZANZIBAR, ALI MOHAMMED SHEIN AREJESHA YA URAIS
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein akionesha Fomu yake ya
kugombea kwa Wanachama wake katika hafla ya kurejesha Fomu hiyo
iliyofanyika katika Viwanja vya Afisi Kuu Kisiwandui. Picha na Makame
Mshenga.
Naibu Katibu Mkuu CCM,Zanzibar
Vuai Ali Vuai akitoa nasaha fupi za kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed mara baada ya kurejesha
Fomu ya kugombea Nafasi ya Urais kupitia chama chake katika Viwanja vya
Afisi hiyo. Picha na Makame Mshenga
Baadhi ya Wanachama waliomdhamini
Dkt. Shein wakifuatilia Hotuba aliyokuwa akiitoa Dkt Shein (hayupo
pichani) katika hafla ya kurejesha Fomu iliyofanyika katika Viwanja vya
Afisi Kuu Kisiwandui.
…………………………………….
Na Faki Mjaka/Maryam Kidiko-Maelezo Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein leo amerejesha Fomu ya
kugombea Nafasi ya Urais kupitia chama chake na kusisitiza kuwa Utulivu
na Amani utaendelea kutawala katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi
Mkuu.
Hatua hiyo imefuata baada ya
kutimiza Vigezo na Masharti yaliyowekwa katika Fomu hiyo na kusema kazi
iliyobaki ni maamuzi ya Chama chake kumpitisha kuwa Mgombea rasmi.
Dkt Shein ameyasema hayo leo Afisi
kuu ya CCM, Zanzibar Kisiwandui alipokuwa akiwahutubia Wanachama
waliohudhuria katika hafla ya kurudisha Fomu.
Dkt. Shein ambaye pia ni Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesema hatomvumilia Mtu
atakayevuruga amani ya Nchi na kwamba Uchaguzi Mkuu usichukuliwe kama ni
kigezo cha kufanya Vurugu Nchini.
“Narudia tena Zanzibar itabaki
kuwa na Utulivu, Amani na Mshikamano na atakayejaribu kuvuruga basi
Vyombo vya Dola vitamshughulikia” Alionya Dkt. Shein.
Amewaasa Vijana kuepuka
kushawishiwa kuivuruga Amani iliyopo na kwamba kufanya hivyo
kutawapelekea kutiwa katika mkondo wa sheria.
Dkt Shein amefahamisha kuwa yeye
na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Kikwete wataendelea kusimamia
Amani na utulivu kama jukumu lao la Msingi.
Kuhusu Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Dkt Shein amesema isitumike kama kigezo cha kuchochea Fujo bali
kila mtu afanye wajibu wake kulingana na Sheria zilizopo.
Amesema nchi inaongozwa na Sheria
na kwamba kila mwenye haki ya kujiandikisha na kupiga kura atapa haki
yake hiyo bila usumbufu wa aina yoyote.
“Nchi inaongozwa na Sheria na
hakuna aliyejuu ya Sheria, hata mimi Rais sipo juu sembuse wingine, kila
mwenye haki ya kupiga kura atapiga bila bughudha yoyote” alisisitiza
Dkt. Shein.
Dkt Shein amewataka Wanachama wenzake kuwa watulivu wakisubiri kumalizika kwa Ilani mpya ya CCM ya Uchaguzi unaokuja.
Awali akimkaribisha Dkt Shein,
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alisema Dkt Shein ametimiza
vigezo vyote vinavyohitajika na kwamba furaha za Wanachama walioshiriki
katika tukio hilo zinaashiria ushindi katika uchaguzi unaokuja.
Dkt Shein ambaye hana Mpizani
katika Chama chake alichukua Fomu June18, na kurudisha leo June 30.
Aidha amedhaminiwa na jumla ya Wanachama 450 wa Unguja na Pemba kutoka
Wanachama 250 ambao ndio Shati la msingi la udhamini.
Post a Comment