HUDUMA YA MADAKTARI BINGWA, YAZINDULIWA MKOANI SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga 
akisalimiana na mmoja wa madaktari bingwa Dokta Vicencia Sakware ( 
Mtaalamu wa Dawa za Usingizi na Wagonjwa Mahututi)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa 
Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael Mhando akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa 
Shinyanga vifaa tiba vitakavyotumika katika zoezi hilo la siku tano.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiagana
 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bwana Michael Mhando na Mkurugenzi wa 
Huduma za Tiba na Ushauri wa KItaalamu Dokta Frank Lekey baada ya 
uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa.
 
 …………………………………………………………….
Akizungumza kuhusu mpango huo wa 
kupeleka madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni, Kaimu Mkurugenzi 
Mkuu wa NHIF Bwana Michael Mhando amesema Mfuko unatekeleza mpango huo 
ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kupeleka huduma bora za matibabu 
kwa wananchi wote. Ameongeza kuwa utekelezaji wa mpango huo unakusudia 
kuwapunguzia wananchi wamikoa ya pembezoni gharama za kufuata huduma 
hizo katika hospitali kubwa ambazo ziko mbali na maeneo wanayoishi.
 
Hadi sasa mpango huo umeshatekelezwa katika mikoa ya Lindi, 
Kigoma, Rukwa, Katavi, Pwani, Tabora, Mara Manyara na Mtwara na 
kuwanufaisha zaidi ya wananchi 7800.
Katiba hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa
 Shinyanga amewapongeza madaktari bingwa hao kwa moyo wao wa kujitolea 
na kuwataka wengine kuiga mfano wao. Aidha amemwagiza Mganga Mkuu wa 
mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa vifaa tiba vilivyotolewa na NHIF 
viendelee kutunzwa ili viwanufaishe wananchi wengi zaidi.
 
Bwan Rufunga pia amewahimiza wananchi wa mkoa wa Shinyanga 
kujiunga kwa wingi katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waondokane na
 unyonge wa kutibiwa kwa kutumiwa fedha taslimu na badala yake watibiwe 
kwa kutumia kadi za CHF.



Post a Comment