Header Ads

Wakazi Jijini Arusha Wajitokeza Kupima Afya Zao Bure

 Baadhi ya wananchi  wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka kcmc pamoja na Mounti meru Hospital ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake duniani  ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide.

 Baadhi ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa  ,Ukimwi na mengineyo.

Mmoja wa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani  viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
...............................

 Na Woinde Shizza,Arusha

Maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha  ambapo wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure.

zoezi hilo ambalo limeanza leo jijini hapa katika kiwanja cha sheikh Amri Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi kwani zaidi ya wananchi 100 wamejotokeza kupima afya zao   bure katika viwanja hivyo.

Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa maathimisho hayo ya wiki ya wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha mkurugenzi wa Phide Intantament Phidesia Mwakitalima alisem akuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza kujitokeza kwa wingi. 

Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao  hivyo ni jambo zuri mno. 

Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na  tabia ya kupima afya zao hadi pale wanapoumwa kitu ambacho sio kizuri na kuwataka wananchi  kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara.

Zoezi hili la kupima afya limeanza leo na linatarajiwa kumalizika march nane na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake.

No comments

Powered by Blogger.