Header Ads

Naibu Waziri MASAUNI awaagiza Maafisa Magereza Kuongeza Kasi ya Uzalishaji

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. 
..................................

Suleiman Msuya

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni amesem Serikali haitasita kuchukua hatua kwa wakuu wa magereza nchini ambao watashindwa kutimiza dhana ya uzalishaji mali ambayo ni agizo la Rais John Magufuli.

Masuani alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa wakuu wa vituo vya magereza Tanzania Bara uliofanyika katika Bwalo la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri alisema iwapo wakuu wa magereza watatumia wafungwa waliopo uzalishaji utaongezeka hivyo kuondokana na tabia ya kulalamika ufinyu wa bajeti.

Alisema pamoja na vigezo mbalimbali vya kupima wakuu wa magereza kigezo kingine kitakuwa ni kuangalia kasi ya uzalishaji kwa eneo husika.

Masauni alisema jeshi la magereza lina rasilimali nyingi kama mashamba na viwanda hivyo wanapaswa kutumia fursa iliyopo kuongeza uzalishaji na kuchochea uchumi wa viwanda.

“Napenda kuwa muwazi hatutavumilia mkuu yeyote wa gereza ambaye atashindwa kuzalisha na kuendeleza fursa ambazo zinamzunguka kwani Tanzania ya viwanda itafanikiwa kupitia vyombo vilivyopo katika wizara yetu,” alisema.



Alisema katika kutatua changamoto ta usafiri wanatarajia kupokea magari 450 siku za karibuni katiya 905 ambayo wameahidiwa na Serikali hali ambayo itaweza kutatua changamoto hiyo.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. 

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. 

Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa  magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga (kulia waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo, mara baada ya Naibu Waziri huyo, kuufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.