Header Ads

Waziri wa Habari akabidhiwa Ripoti na Kamati ya Uchunguzi wa Tukio lililotokea CLOUDS

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Hassan Abbass.

Katibu wa Kamati ya Kuchunguza Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Kituo cha Televisheni cha Clouds Media, Deodatus Balile akielezea yaliyomo katika ripoti yao kabla ya kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nauye (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam, Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Dkt. Hassan Abbass na Katibu wa Kamati hiyo Deodatus Balile.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akikabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa sakata hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass leo Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha Televisheni cha Clouds Media ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye ushahidi wa CCTV uliombatanishwa katika CD aliyomkabidhi leo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia makabidhiano ya ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.