Header Ads

KASSIM MAJALIWA: Tanzania ina Utashi wa Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Biashara

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua mkutano wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius mjini Port Louis nchini Mauritius , Machi 23, 2017.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji  kati ya Tanzania na Mauritius wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua  mkutano huo mjini Port  Louis  Machi 23, 2017.
......................................................


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli inautashi wa dhati wa kuboresha mazingira ya uwekezani na biashara nchini kwa kuondoa rushwa na urasimu katika sekta ya umma, hivyo amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Mauritius kuja nchini.

Amesema Tanzania imefanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa kubadili mifumo yake ya kisheria, kitaasisi na kifedha ili kuhakikisha wawekezaji wanahudumiwa ipasavyo na kupewa umuhimu wanaostahili kwani ni wadau muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Waziri Mkuu amesema hayo jana wakati akifungua  kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius lilifanyika katika Hotel ya Labourdonnaise mjini  Port Louis nchini Mauritius. Kongamano hilo  liliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

“Kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli nawakaribisha kwa mikono miwili kuja na kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda na utalii na kutembelea vivutio vya utalii na kupata burudani ya aina yake na kwa wafanyabiashara Tanzania ni mahali pazuri kwa kuwekeza,” alisema.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Mauritius Mheshimiwa Pravind Kumar Jugnauth, Prime Minister of the Republic of Mauritius; Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius.

Wengine ni Mwenyekiti wa ‪Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye,, Executive Director of Tanzania Investiment Centre; ‪Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Clifford Tandar pamoja na Maofisa wa Serikali ya Tanzania na Mauritus.

Waziri Mkuu wa Mauritius, Bw. Pravind  Kumar Jugnauth akizungumza katika mkutano wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius mjini Port Louis Machi 23, 2017. 

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji  kati ya Tanzania na Mauritius wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Mauritius, Bw. Pravind  Kumar Jugnauth akihutubia kwenye mkutano huo mjini Port  Louis  Machi 23, 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri Mkuu wa Mauritius, Bw. Pravind Kumar Jugnauth katika mkutano wa Uwekezaji na Biashara kati ya Tanzania na Mauritius kabla ya kufungua mkutano huo mjini Port Louis, Machi 23, 2017.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments

Powered by Blogger.