Header Ads

Serikali yaunda Kamati Kuchunguza Mkasa Uliotokea CLOUDS MEDIA GROUP


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya watu watano kuchunguza suala la kilichotokea Clouds Media siku ya Alhamisi pamoja na Ijumaa usiku.

Kamati hiyo imeundwa baada ya Waziri Nape kufanya ziara Clouds Media leo Jumatatu 20/03/2017 na kuzungumza na uongozi wa Clouds Media kufuatia tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutembelea ofisi hizo siku ya Ijumaa usiku akiwa na askari wenye silaha.

Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Dkt. Hassan Abbas Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Deodatusi Balile Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Ndg. Jesse Kwayu Mhariri Mtendaji Gazeti la Nipashe, Ndg. Mengida Johannes kutoka Wapo Redio pamoja Ndg. Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Baada ya kamati hii kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kutoka pande zote mbili Wizara itasema hatua itakazochukua.  

Imetolewa na:
Zawadi Msalla
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

20/03/2017

No comments

Powered by Blogger.