Header Ads

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa MAGHEMBE akutana na Mbobezi wa Picha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akikabidhiwa kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba la Selous na Mtaalamu wa picha wa  Kimataifa, Bw. Robert Ross wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini  Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo  katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Mhe. Waziri ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu , Injinia Angelina Madete, katika Hoteli ya Slip way. Kitabu hicho kinatarajiwa kutumika  kama nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa.
mag3 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiangalia baadhi ya picha katika kitabu cha picha za wanyamapori  waliopo katika Pori la Akiba la Selous na mara baada ya kukabidhiwa kitabu hicho na  Mtaalamu Kimataifa, Bw. Robert Ross (kushoto)  wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini  Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo  katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo jioni katika Hoteli ambapo Kitabu hicho kitakuwa ni nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania  katika Nyanja za Kimataifa.
mag4 
Huu ni mwonekano wa nje wa kitabu cha Picha  zilizochukuliwa katika Pori la Akiba Selous na Mtaalamu wa picha wa  Kimataifa, Bw. Robert Ross, Kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri, Prof. Maghembe ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Injinia Angelina Madete  katika hoteli ya Slipway.

No comments

Powered by Blogger.