Header Ads

Profesa MBARAWA akagua Upanuzi wa Uwanja wa Ndege Mjini DODOMA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi miwili kwa mkandarasi Chicco anaefanya upanuzi wa njia ya kuruka na kutua ndege katika uwanja wa ndege wa dodoma kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua kazi ya upanuzi wa uwanja huo, Prof. Mbarawa amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa ujenzi wa uwanja huo unafanyika kwa kuzingatia viwango vilivyokubalika katika mkataba na kuukabidhi kwa wakati.

“Hakikisheni upanuzi huu unakamilika kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja wa ndege wa Dodoma,hasa mkizingatia umuhimu wake kitaifa’, amesema Prof. Mbarawa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Kampuni ya Chico, anayefanya upanuzi wa njia ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa ndege wa Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Miradi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. Mbila Mdemu ( wa pili kulia), wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma.

Naye Mkandarasi anaejenga uwanja huo amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa atahakikisha ujenzi wake unazingatia viwango na kuukabidhi katika muda uliokubalika kimkataba.

Zaidi ya shilingi bilioni 11.8  zinatarajiwa kutumia katika upanuzi huo na hivyo kuwezesha ndege nyingi zaidi kutumia uwanja huo.
Ujenzi wa Barabara ya Kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa ndege wa Dodoma ukiendelea, Ujenzi huo kwa kiwango cha lami unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi miwili.

No comments

Powered by Blogger.