Header Ads

Mgodi wa Dhahabu wa Geita wakabidhi Vifaa vya Watoto Hospitali ya Muhimbili

Na Neema Mwangomo

Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH)  leo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya watoto vyenye thamani ya Shilingi Milioni 23 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita  (GGM).
Msaada huo umetolewa kupitia chama cha Madaktari wa watoto Tanzania.

Vifaa vilivyotolewa ni BP Machine 10, Infusion Pump 2, Thermometers 110, Standing Weighing Scales 6, Lying Down Weighing Scales 6, Nebulies 3 pamoja na Pulse Oxymeter 10.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa  GGM, Terry Mulpeter,  Daktari Mkuu wa mgodi wa GGM,  Kiva Mvungi amesema lengo ni kuwa sehemu ya jamii, lakini pia kutambua juhudi zinazofanywa na madaktari wa watoto katika kuboresha huduma za afya.

“GGM kama mdau katika sekta ya afya imeamua kutoa msaada huu ili watoto na kina mama watakaofika Muhimbili waweze kupata huduma hizi muhimu  kwani tunatambua changamoto mnazopata katika kuwahudumia watoto, lakini pia tunatambua mchango wenu,” amesema Daktari Mvungi.
Daktari wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi (kulia) akikabidhi LEO msaada wa vifaa vya watoto kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha (kushoto) wa Hospitali hiyo, Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Merry Charles na katikati ni Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa GGM, Tenga Tenga wakishuhudia tukio hilo.
Daktari wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi (kulia) akikabidhi LEO msaada wa vifaa vya watoto kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha (kushoto). Kutoka Kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari wa Watoto, Dk Namala Mkopi, Dk Merry Charles na Tenga Tenga (kulia) akishudia tukio hilo leo.
 Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Tiba MNH ambaye  ni Mkuu wa Idara ya Watoto, Daktari Mary Charles amesema msaada huo  umekuja wakati muafaka kwani vifaa hivi ni muhimu na vinahitajika kwa ajili ya kuwahudumia watoto .

“Tunawashukuru GGM  kwa msaada wenu  ni vifaa muhimu sana kwani unapotaka kumpatia dawa mtoto hauangalii umri bali unaangalia uzito wake hivyo unampima uzito kwanza  alafu  unampatia  dawa kulingana na uzito  wake” Amesema Dk. Charles.

Kwa mujibu wa Dk Charles  jengo la watoto  hulaza watoto  300 ambapo pia kila kliniki ina uwezo wa kuchukua watoto 60.

No comments

Powered by Blogger.