Header Ads

Mv MAGOGONI kukamilika Mwezi Agosti Mwaka Huu

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua ukarabati na Ujenzi wa Vivuko vya MV Magogoni na MV Pangani na kuwataka wajenzi wa vivuko hivyo kuhakikisha vinakamilika kwa wakati.

Akizungumza mara baada ya kuvikagua Vivuko vya Old MV-Magogoni na Ujenzi wa vivuko vipya vya Pangani na New Magogoni, Prof. Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na hatua za ujenzi zilizofikiwa na kusisitiza kuwa upo umuhimu wakazi hizo kufanywa hapa hapa nchini badala ya kupelekwa nje ya nchi.

“Hakikisheni mnaongeza nguvu na wataalam ili kazi zote za vivuko na ujenzi wa boti za kuongozea Meli (Tag), zifanyike hapa hapa nchini na hivyo kuokoa fedha nyingi zinazotumika kila mwaka kwa Tag zote saba kukarabati wa nje ya nchi”, Amesema Prof. Mbarawa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase wakati alipokagua mradi wa ukarabati wa ujenzi wa vivuko vitatu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Prof. Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase wakati alipokagua mradi wa ukarabati wa ujenzi wa vivuko vitatu jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Kivuko cha MV Magogoni kikiwa kwenye hatua za mwisho za matengezo yanayofanywa na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya Mwanza na TEMESA Jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.