Header Ads

Rais Dkt MAGUFULI afuturisha Makundi ya Viongozi wa Dini na Walemavu wa Ngozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dkt Magufuli amefuturisha makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu wa ngozi Albino, Wavuvi wa ferry, walemavu vya viungo pamoja na wafanyakazi wa Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir wakati wakielekea kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na makundi mbalimbali (hawapo pichani)ikiwemo viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu wa ngozi (Albino),walemavu wa viungo pamoja na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyetambulika kwa jina moja la Yusuph mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.