Header Ads

Rais Dkt MAGUFULI akabidhiwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali  mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi(NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Uchaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwanasiasa mkongwe John Shibuda huku Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein naye akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo mara baada ya kukamilika kwa tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi. 
Baadhi ya Wageni na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupokea taarifa hiyo ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

PICHA NA IKULU

No comments

Powered by Blogger.