Header Ads

Mamlaka ya Elimu TANZANIA yapongeza Kwa Kuinua Sekta ya Elimu Nchini

Na Hassan Silayo

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Same Herman Kapufi ameshukuru Jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kutekeleza miradi inayosaidia kuongeza ubora wa elimu nchini.

Ikiwemo utekelezaji wa mradi kukarabati shule kongwe nchini utakaoboresha mazingira ya kufundishia na kusaidia kuinua kiwango cha elimu katika shule hizo.

Mh. Kapufi amesema kuwa mpango huo umekuja wakati muafaka wakati uongozi wa wilaya hiyo ukipambana kutatua changamoto za elimu na kuwataka wadau kuipa ushirikiano Mamlaka hiyo.

“Kwa kweli napenda kuishukuru Mamlaka ya elimu Tanzania kwa jitihada zake hizi za kuboresha sekta ya elimu nchini, kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana katika wilaya hii kwa kipindi chote nilichokuwa hapa kama mkuu wa wilaya, shule zetu kongwe zimechoka sana na zinahitaji ukarabati ili kuweza kuzirudisha katika hali yake ya kawaida kwa utekelezaji wa mpango huu” Alisema Mh.Kapufi.

Naye Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bibi. Sylvia Lupembe amesema kuwa kupitia TEA mpango huo utatekelezwa katika shule kongwe 11 katika mikoa ya Bukoba, Mwanza, Tabora, Singida, Same, Arusha, Dodoma, Morogoro na Pwani kwa kuzifanyia ukarabati wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo madarasa, vyoo, maabara, mabweni na mifumo ya umeme.

“hali ya shule zetu kongwe kwa kweli sio nzuri tumetembea kwenye mikoa takribani Mikoa sita tumejionea halihalisi ya miundombinu ya shule zetu kongwe hazipo katika mazingira mazuri ya kujifunzia kutokana na kuwa na miundombinu chakavu na kwa mradi huu tunataka kuweka mazingira mazuri ya watoto wetu hawa kujifunzia hasa kwa kuanza na shule hizi kongwe” Alisema Sylvia.

Wakizungumzia ukarabati huo Mwalimu Mkuu wa shule wa Shule ya Sekondari Nganza Bi. Yacinta Lyimo aliishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa Utekelezaji wa mpango huo kwani utasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na hata kusaidia kuinua kiwango cha elimu  na ufaulu katika shule hizo.

Aidha, Afisa Elimu wa Manispaa ya Singida Bw. Omari Kisuda Mpango huu wa maboresho ya shule kongwe ni mkombozi katika sekta ya elimu na umekuja wakati uhitaji wa maboresho ya shule hizo unahitajika hasa kutokana na baadhi ya shule kushindwa kufanya ukarabati wa mara kwa mara kutokana na ufinyu wa bajeti.


No comments

Powered by Blogger.