Header Ads

Michuano ya COPA AMERICA yafikia Hatua ya Robo Fainali


Na Mwandishi Wetu

 MICHUANO ya Copa America inayoonekana moja kwa moja kupitia visimbuzi vya StarTimes Tanzania imefikia hatua ya robo fainali ambayo itaanza kutimua vumbi kesho Juni 16 mpaka 19.

Timu zilizotinga hatua hiyo ni Argentina, Chile, Mexico, Marekani, Venezuela, Peru, Colombia na Ecuador huku mashabiki wa soka wakishuhudia miamba ya soka ya timu za Brazil na Uruguay wenye nyota lukuki kama vile Luis Suarez, Edinson Cavani, Willian, Countinho na wengineo wakishindwa kuzisaidia timu zao.

Katika michuano hii ya kusisimua kikosi cha timu ya taifa cha Argentina kikiongozwa na mchezaji bora wa dunia mara tano, Lionel Messi, ambacho kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kimeingia kwa kishindo hatua ya robo fainali baada kushinda michezo yote mitatu na kuongoza kundi D kwa alama tisa.

Hatua ya robo fainali itakayoanza kupigwa kesho itazijumuisha timu zote zilizoshika nafasi ya pili katika makundi yao.

Wapenzi wa soka ulimwenguni wanazidi kusononeshwa na mwenedo mbovu wa kikosi cha taifa cha Brazil ambacho kimeshindwa kutinga hatua hiyo kwa kufanikiwa kushinda mechi moja tu kati ya tatu. Matokea hayo mabovu yamepelekea kocha wa taifa timu hiyo Dunga kutimuliwa kazi.

Timu na ratiba kwa timu zitakazopambana ni  pamoja na Marekani na Ecuador (Juni 16), Peru na Colombia (Juni 17), na mechi za mwisho ni Argentina na Venezuela; Mexico na Chile (Juni 18). Timu zitakazopita hatua hii zitakutana katika hatua ya nusu fainali siku ya Juni 21.

No comments

Powered by Blogger.