Header Ads

Hospitali ya Rufaa ya IRINGA yapewa Mwezi Mmoja kutafuta Ufumbuzi wa Taka Hatarishi


Na Mwandishi wetu, Iringa

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa, Mkoani Iringa Kulitaftia ufumbuzi suala la uteketezaji wa taka ngumu katika hospitali hiyo.

Mh. Mpina ametoa maagizo hayo leo alipotembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa  wa Iringa katika ziara yake ya kukagua usafi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa maziringa katika viwanda vya mkoa wa Iringa.

Imeelezwa kuwa uteketezaji wa tanga hatarishi katika hosptali hiyo ya mkoa umekumbana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa kifaa cha kuteketeza taka hospitalini hapo kwa muda mrefu bila matengezo yeyote uliosababishwa na taratibu za utekelezaji manunuzi serikalini.

Kulia Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Iringa dkt Robert Salim, akitoa maelezo ya uteketezaji wa taka katika hospatali ya Rufaa kwa  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina na Ujumbe wake walipokagua mazingira ya hosptali hiyo leo.
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Mh luhaga Mpina , kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Charles Kasesera Kulia Naibu Meya wa mji wa Iringa Bw. Joseph Liata ambae pia ni diwani (Chadema) kwa pamoja wakifanya usafi katika soko la mji wa Iringa.
Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina wakimwaga maji wakati wakifanya usafi sokoni Mkoani Iringa Leo.
..................................


Kwa Upande wake mganga mkuu mfawidhi wa hospital hiyo dkt Robert Salim Amemueleza Naibu waziri Mpina kuwa taka zizalishwazo katika hosptali hiyo zimekuwa zikitupwa katika Dampo la mkoani hapo na hata hivyo..hosptali imekuwa na wakati mgumu sana katika kuteketeza taka hatarishi kama vile za sindano, gloves, nyembe na bandeji mana haziozi ardhini kirahisi.

Akitolea ufafanunuzi sualala za uteketezaji wa taka hatarishi hospitalini hapo, mratibu wa kanda ya nyanda za juu kusini wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) bw. Godlove Mwamsojo..ameleeza kuwa baraza limewahi kushauri uongozi wa hosptali hiyo kuteketeza taka hizo kwa kusaidiwa na kiwanda cha mbao cha Sao hill kilichopo wilayani Mufindi kwa kuwa kiwanda hicho kina vifaa vya kutosha, bila mafanikio kutokana na sababu kwamba hospital hiyo huzalisha taka nyingi kuzidi uwezo wa kiwanda cha Sao Hill kusaidia kuziharibu.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Mpina alikagua mazingira ya soko la Mjini Iringa na kushiriki katika usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti, ambapo  Mh. Mpina,alipanda mti katika kata ya Kitwivu na kuwaasa wakazi wa Iringa kuwa walinzi wa misitu na kutoa taarifa za wizi na uhujumu wa magogo ili sheria ichukue mkondo wake na kuwaasa watunze vyanzo vya maji kama walivyotunza vizuri chanzo cha maji ya chemchem cha Kitwivu.

“Taifa lazima lipande miti ili kuhepukana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi tunazokumbana nazo.” Alisisitiza. Aidha Mh Mpina aliiongeza Wilaya ya Mufindi kwa kupitiliza lengo la kupanda miti milioni moja na laki tano kila mwaka katika kila wilaya na kupanda miti milioni thelathini na tano kwa mwaka.
Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.  Luhaga Mpina Akipanda mti kabla ya kuupanda , katika eneo la chanzo cha maji cha Kitwiru Mkoani Iringa.
Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.  Luhaga Mpina Akipanda mti kabla ya kuupanda , katika eneo la chanzo cha maji cha Kitwiru Mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiuumwagilia na kuusindilia mti baada ya kuupanda katika eneo la chanzo cha maji ya chemchem cha Kitwiru Mkoani Iringa.

(Picha na habari  na Evelyn Mkokoi)

No comments

Powered by Blogger.