Mtambo wa Kusukuma Maji Kutoka Ruvu Chini Kwenda Jijini Dar es Salaam Wawashwa Kwa Majaribio
Sehemu ya maungio
ya Mabomba yanayoingiza maji ndani ya Mtambo huo kutoka mto Ruvu, chini.
|
Moja ya maungio ya
Bomba kubwa la kusafirishia Maji kutoka mtambo wa Maji wa Maji wa Ruvu Chini,
Bagamoyo Pwani lililoko eneo la Tegeta jijini Dar es salaam likiwa
limekamilika.
|
Sehemu ya ndani ya Matenki yanayopokea maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini yaliyoko eneo la Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es salaam. |
Na. Aron Msigwa – MAELEZO
Hatimaye moja ya Pampu
kubwa katika mtambo wa kuzalisha Maji kwenye chanzo cha maji cha Ruvu Chini,
Bagamoyo mkoani Pwani imewashwa kwa majaribio kufuatia kukamilika kwamradi wa ujenzi
wa bomba kubwa la kusafirishia maji lenye urefu wa kilometa 55.9 kutoka chanzo
hicho kwenda jijini Dar es salaam.
Majaribiohayo ni
sehemu ya awali ya kupitisha maji yenye msukumo mkubwa kwenye bomba hilokuelekea
kwenye matenki makubwa ya kuhifadhia maji yaliyoko eneo la Chuo Kikuu Ardhi
jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara
baada ya kuwasha Pampu hiyo Katibu Mkuu waWizara ya Maji na Umwagiliaji Muhandisi
Mbogo Futakamaba amesema kuwa majaribio hayo ambayo yameonyesha mafanikio yatawawezesha
wakazi wa jiji hilo na maeneo ya mkoa wa Pwani kupata huduma ya uhakika ya Maji
kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.
Amesema mradi huo utakuwa
suluhisho la tatizo la maji la muda mrefu kwa kuwa kiwango cha maji kitakachozalishwa kwa
siku kitafikialita milioni 270 ambazo zitaongezwa kwenye msukumo wa lita milioni
182 zilizokuwa zikizalishwa hapo awali kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba
hilo.
“Hii ni faraja kwa
Serikali na wakazi wa jiji la Dar es salaam na mkoa wa Pwani, sasa tutapata
lita Zaidi ya milioni 270 kwa siku haya ni mafanikio makubwa, kulingana na
mahitaji tuliyokuwa nayo tutahakikisha tunayasambaza maji haya ili kukidhi mahitaji
ya wananchi” Amesema Muhandisi Futakamba.
Muhandis Futakamba
amewataka wahandisi na watendaji wanaosimamia uendeshaji wa mitambo hiyo kuwa
mahili na makini katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuhakikisha inafanya
kazi kwa ufanisi na kwa maslahi ya umma.
Ameiagiza DAWASA
na DAWASCO kuendelea kuwajengea uwezo kielimu Wahandisi wa ndani wanaohusika na
utunzaji wa miundombinu hiyo ili miradi ya maji wanayoisimamia iweze kudumu na
kuwa endelevu kupitia matengenezo na huduma mbalimbali watakazozifanya.
“Ninyi kama
wahandisi na wasimamizi wa miradi na mitambo hii mikubwa hakikisheni mnajenga uwezo wenu wa ndani ili muweze kuiendesha
na kuidhibiti mitambo hii pia kuwa na uelewa wa ndani wa mifumo yote
iliyotumiwa wakati wa uwekaji wake na mabadiliko ya teknolojia” Amesisitiza.
Pia amewataka
watendaji hao kuhakikisha kuwa wanatunza mitambo na miundombinu yote ya majiili
iweze kudumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwanufaisha wananchi wengi zaidi.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Muhandisi Archard
Mutalemwa akizungumza mara baada ya kukagua mitambo ya kuzalisha Maji ya Ruvu
Chini amesema kuwa kukamilika kwa bomba hilo ni mwendelezo wa juhudi za
Serikali kupitia DAWASA za kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma ya maji
Safi.
Amesema DAWASA
itaendelea kutekeleza majukumu yakekwa kuhakikisha inaendeleza na kusimamia
miradi ya maji ikishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo na kuhakikisha inawawezesha
wakazi wa jiji la Dar es salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani yanapata huduma ya Maji
Safi kupitia miradi iliyochini yake.
Naye Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO)
Muhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza mara baada ya kuwashwa kwa mtambo huo
amesema kuwa DAWASCO imejipanga kuhakikisha inawasambazia huduma ya maji wakazi
wengi zaidi wa jiji hilo ambao walikua na miundombinu lakini hawapati huduma
hiyo pamoja na kuunganisha wateja wapya kwa gharama nafuu.
“Naishukuru
Serikali kwa kuwezesha mafanikio haya sisi kama DAWASCO tumejipanga na
tutahakikisha maji yanayozalishwa yanawafikia wananchi, yapo maeneo mengi
yaliyokuwa na changamoto ya huduma hiyo hata yale ambayo yalikua yameunganishwa
tayari katikati ya jiji nay ale yaliyo pembezoni mwa jiji tutahakikisha
tutayafikia” Amesisitiza.
Akizungumzia hatua
zinazochukuliwa kudhibiti wa wizi wa maji amesema DAWASCO imeanzisha maeneo 25 (DMA)
ambayo yamefungwa mita kubwa katika wilaya za jiji hilo ili kuwawezesha Mameneja
wa Zoni husika kuweza kubaini wizi , upotevu wa maji, ubovu wa mita na tatizo
la usomaji na kisha kuchukua hatua kwa wale wanaobainika kuhujumu miundombinu
hiyo.
Aidha, amesema
DAWASCO imeandaa mpango wa kuziondoa mita zoteambazo zimefikia umri wa miaka 10
ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa mradi
wa ujenzi wa bomba kubwa la kusafirishia maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini wenye
urefu wa kilometa 55.9 umejengwa na Kampuni ya JBG Gauff Ingenieure kwa gharama
ya shilingi Bilioni 141 ambazo zote zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Post a Comment